JAMII YASHAURIWA KURUDISHA MALEZI YA ZAMAN.
NA FATMA HAMAD Mjumbe wa kamati tendaji wa jumuia ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Wete Faki Khamis Simai ameitaka jamii kurudisha malezi ya pamoja katika kuwalea watoto wao jambo ambalo litapelekea kupatikana kwa kizazi chenye madili mema. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko katika ofisi za wasaidizi wa sheria wilaya ya wete [WEPO] amesema asilimia kubwa ya madili ya wazanzibar yameporomoka ukilinganisha na miaka ya nyuma ‘’Zamani watoto walikua ni wa watu wote hakukua na mtoto wa Fulani wala wa Fulani akifanya kosa anahukumiwa ni mtu yoyote wala hakuna tatizo lolote’’ alisema Faki Simai. Hivyo ni wakati wazazi kuamka na kukshirikiana kwa pamoja ili kurudisha malezi ya zamani jambo ambalo litakua ni muarubaini wa kupunguza mmongonyoko wa madili ya wazanzibar na kupelekea watu kuishi wakiwa na hkofu ya Allah [A,T]. Aidha kwa upande mwengine ameitaka jamii kuwacha tabia ya kuzificha na k