JAMII YASHAURIWA KURUDISHA MALEZI YA ZAMAN.

 




                                 NA FATMA HAMAD 

Mjumbe wa kamati tendaji wa jumuia ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Wete Faki Khamis Simai  ameitaka jamii kurudisha  malezi ya  pamoja  katika kuwalea  watoto  wao  jambo  ambalo  litapelekea  kupatikana  kwa  kizazi  chenye  madili  mema.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi  huko katika ofisi za wasaidizi wa sheria wilaya ya wete [WEPO]  amesema    asilimia kubwa ya madili  ya wazanzibar   yameporomoka   ukilinganisha na  miaka ya  nyuma

‘’Zamani   watoto  walikua ni  wa watu wote hakukua na mtoto  wa  Fulani wala  wa Fulani akifanya kosa anahukumiwa ni  mtu yoyote  wala hakuna tatizo lolote’’ alisema Faki Simai.

Hivyo  ni  wakati   wazazi   kuamka  na  kukshirikiana   kwa pamoja  ili   kurudisha  malezi  ya  zamani  jambo ambalo litakua ni muarubaini wa kupunguza  mmongonyoko wa madili ya  wazanzibar  na kupelekea watu kuishi wakiwa na hkofu ya Allah [A,T].

Aidha kwa upande mwengine ameitaka jamii kuwacha tabia ya kuzificha na kuzifanyia suluhu wenyewe kwa wenyewe  kesi za udhalilishaji jambo ambalo litasaidia kuendelea kwa matukio ya udhalilishaji wa wanawake na watoto ndani ya Nchi.

Kwa upande wake afisa mipango kutoka jumuia  ya wasaidizi wa sheria wilaya ya wete  Salim Hamad Salim amewataka viongozi wa dini kushirikiana na wasaidizi wa sheria kuielimisha jamii ili kuona wanakuwa mstari wa mbele kupiga vita vitendo viovu ikiwemo udhalilishaji wa kijinsia, ubakaji na ujambazi.

 ‘’Viongozi wa dini na nyinyi mnamchango mkubwa katika kuhakikisha jamii inaishi kwa amani bila ya kuepo na matatizo yoyote’’ alieleza afisa mipango.

Nae mkurugenzi wa jumuia  hiyo Hemed Ali Hemed amewataka wasaidizi wa sheria wasivunjike moyo bali waendelee kuielimisha jamii ili kuhakikisha wanaifahamu sheria na kuweza  kudai haki zao wakati  zitakapo vunjwa.


Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.