DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO

 


                     NA FATMA HAMAD – PEMBA

SHAHIDI  BASHE  MAKAME  Khamis  ambae  ni Afisa kutoka Maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali  Zanzibar ameiambia Mahkama ya Mkoa iliyopo Wete  Kaskazi Pemba, k baada ya kufanya uchunguzi wa vinasaba katika Mashine ya DNA vipimo vimengudua kwamba mtuhumiwa Bahati  Mashauri ndie baba mzazi wa mtoto aliezaliwa na binti aliembaka.

Akitoa ushahidi wake  mbele ya Mahkama hiyo ya Mkoa  Bashe alidai kuwa baada ya kupokea vinasaba vya mtoto aliezaliwa na vya mtuhumiwa  pamoja na mama aliezaa baada ya kubakwa, alianza kufanya uchunguzi wa  vinasaba  vya mtoto na mtuhumiwa  na kugudua kwamba mtuhumiwa  ndie baba  mzazi wa mtoto kwa asilimia 9.99

Aidha alidai kuwa  aliendelea  kufanya vipimo  vya  vinasaba vya mtoto na mama yake  pia aligundua kwamba  mtoto ndie mama yake mzazi binti ambae amedaiwa kubakwa.

‘’Baada ya kufanya uchunguzi wa vinasaba vya mtuhumiwa, mtoto na mama kipimo chetu cha DNA kiligundua kwamba mtuhumiwa ndie baba mzazi wa mtoto, na yule binte ndie mama wa mtoto,’’alidai.

Alidai kuwa kwa mujibu wa majibu walioyagundua katika vipimo vyao ni wazi kwamba mtuhumiwa anaedaiwa kubaka  ndie baba mzazi wa mtoto.

 Baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake huo shahidi huyo, Mwendesha Mashtaka wa Serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka  (DPP )  Juma  Mussa   Omar  alidai  walikua wamebakiwa  na  shahidi  huyo  mmoja na wanafunga ushahidi  hivyo  alimtaka Hakimu anaendesha kesi hiyo kuighairisha na kuipanga siku nyengine kwa ajili ya kuendelea na hatua nyengine.

‘’Mheshimiwa Hakimu sisi tulikua tumebakiwa na shahidi huyo mmoja na leo tunafunga ushahidi, hivyo tunaomba uighairishe hadi sikunyengine,’’alidai.

Nae Hakimu wa Mahkama hiyo ya Mkoa ambae ndie anaeisikiliza kesi hiyo  Zuwena Mohamed Abdulkadir alikubaliana na ombi la upande wa mashataka, na aliighairisha hadi April 15 mwezi huu kwa hatua ya utetezi.

‘’Mtuhumiwa naipanga tarehe  hiyo  ya 15  ili  tuje  tuone  kama una  la  kujibu  ama  laa,’’alieleza.

Ilidaiwa Mahkamani hapo mtuhumiwa huyo baina ya mwezi wa Mei na Juni mwaka jana majira ya saa 12:00  za  usiku, katika kijiji cha Gando Chaoni Wete Pemba,  alimbaka msichana wa miaka 14.

 Ambapo kufanya kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 108 (1) (2) (e) na 109 (1) vya sheria ya adhabu, nambari 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar.

 

Comments

Popular posts from this blog

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

‘’KATIBU MKUU ELIMU ‘’TOENI ELIMU YA MALEZI BORA’’