Posts

Showing posts with the label WANAWAKE

WAJASIRIAMALI WATAKIWA KUJIUNGA NA MAJUKWAA YA WANAWAKE

Image
  NA, FATMA HAMAD-PEMBA Mkurugenzi  Idara ya Maendeleo  ya Jamii Jinsia wazee na Watoto Zanzibar Siti Abasi Ali amewataka Viongozi wa Majukwaa ya Wajasiriamli Wanawake Kisiwani Pemba kuhakikisha wanavishajihisha Vikundi Vya Ujasiriamali kujiunga na Majukwaa hayo  ili viweze kuwezeshwa kwa  kupatiwa mikopo ya kujiendeleza kiuchumi. Mkurugenzi  huyo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wenyeviti wa Majukwaa wa wilaya Nne za Pemba katika hafla ya ufunguzi wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo wajasiria mali hao. Alisema Vikundi vitakapo jiunga na majukwaa hayo itakuwa rahisi kupatiwa mikopo ya kujiendeleza katika harakati zao . Alisema Serikali imeaanzisha majukwaa ya Wajasiriamali wanawake kwa ajili ya kuwaunganisha Pamoja na kuwa na sauti moja ili waweze kujadili shida walizonazo . Alisema hatua hiyo itakuwa rahisi kuweza kuwafikia kwa wepesi katika kuwasidia kwa kuwapatia mitaji ya kujiendeleza kiuchumi, ili  waondokane na utegemezi na unyanyasi wanaoupata...

Ni ipi nafasi ya familia katika kuwashajiisha watoto wa kike kushiriki michezo.

Image
Na, Fatma Hamad NA FATMA HAMAD, PEMBA Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kupitia idara yake ya michezo, imekuwa ikitoa fursa mbali mbali za kimaendeleo ikiwemo ajira, kushiriki mabonanza nje ya Zanzibar. Hilo limekuja kwa wazazi kutokuwapa nafasi watoto wa kike kushiriki michezo, kwani bado wanahisi kwa mwanamke ni uhuni na kupelekea siku zote kubaki nyuma kimichezo. Licha ya Serikali kutoa fursa nyingi za kimaendeleo, bado ushiriki wa wanawake na watoto wa kike, ni mdogo ukilinganisha na wanaume hapa visiwani Zanzibar, hususan kisiwa cha Pemba. Wazazi na walezi wanayo kila sababu ya kuhakikisha wanawapa nafasi (fursa) watoto wa kike, kushiriki kwenye michezo ili kuona nawao wanajinyakulia fursa zilizomo kwenye Sekta ya michezo. Kwani wapo wengi wamekuwa ni wachezaji wazuri wakati wanapokuwepo skuli, wanapomaliza vipaji hivyo hupotea. Makala hii itangazia nafasi ya wanajamii (familia ) katika kuwashajiisha watoto wa kike, kushiriki ipasavyo kwenye michezo. WATOTO Mtoto F...

WAJASIRIAMALI WATAKIWA KUWANZISHA MIRADI AMBAYO ITAWALETEA MAENDELEO

Image
      NASALIM HAMAD PEMBA. Kaimu mkurugenzi wa Jumuiya ya Wasaidizi wa Sheria wilaya ya Micheweni [Midipao] Saleh Hamad Juma amewataka wajasiriamali kuanzisha miradi kama vile utengenezaji wa Sabuni,Ukulima wa mboga ili waweze kujipatia faida itakao saidia kuendesha vikundi vyao. Ushauri huo ameutoa wakati akizungumza na wanakikundi cha kueka na kukopa cha Hatusemani kilichopo   Tumbe kaliwa wilaya ya Micheweni mkoa wa Kakazini Pemba katika kikao maalumu kilichoandaliwa na jumuiya hiyo cha kuishajiisha jamii kujiunga na vikundi vya ujasiriamali. Alisema endapo watazalisha Sabini, au kujingiza kwenye kilimo cha mboga mboga watajipatia kipato na kukuza vikundi vyao kupiga hatua kimaendeleo. ‘’Niwaombe mama zangu musishie tu kuja mukiweka pesa na kuondoka, bali anzisheni miradi ili muweze kuviendeleza vikundi vyenu pamoja na kujipatia kipato ambacho kitainua maisha yenu, alisema.   Aliendelea kusema endapo watazalisha bidhaa zenye ubora ambazo zitaendana ...