Posts

Showing posts from October, 2026

SERIKALI YAAHIDI KUISUKA SEKTA YA ELIMU

Image
  NA FATMA HAMAD, PEMBA SERIKALI YA MAPINDUZI Zanzibar imesema itaendelea kuboresha miundombinu ya Elimu ikiwemo Majengo, vifaa vya kisasa pamoja na maslahi kwa Walimu, ambavyo vitaibua vipaji na kuleta ufaulu mzuri kwa wanafunzi, wawe  na sifa za kuingia katika soko la ajira. Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu Utawala kutoka wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Amos John Henok  kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo Khamis Abdulla Said, katika maadhimisho ya siku ya Walimu Duniani, huko Skuli ya Sekondari Uweleni Mkoani mkoa wa Kusini Pemba.  Alisema lengo la serikali ya Mapinduzi ni kuona Zanzibar inakua na Wataalamu wengi  na ambao wamebobea katika fani mbalimbali kama vile Walimu, Madaktari, Mainjinia pamoja na wataalamu wa mitandao, hivyo itahakikisha inaboresha miundombinu ya kisasa, ili kufikia azma yake hiyo. ‘’Tutahakikisha tunaendelea kuweka mazingira rafiki katika sekta hii ya Elimu, ili vijana waweze kuuzika katika soko la ajira,’’ alielez...

Jeshi la Polisi lamsaka aliehusika na mauwaji ya mtoto wa kidato cha kwanza

Image
  NA FATMA HAMAD, PEMBA JESHI la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba linaendelea na uchunguzi wa tukio la kuuwawa mtoto wa kike anaejulikana kwa jina la Raiyan Hemed Amour mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa kijiji cha Kwale Mpona shehia ya Finya Wilaya ya Wete, aliekutwa kwenye kichaka amefariki huku kiganja cha mkono wake wa kulia kukatwa na kitu chenye ncha kali. Kamanda wa Polisi Mkoa huyo  Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) William Mwampagale alisema kuwa, marehemu huyo alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika skuli ya Sekondari Kizimbani Wete, ambapo kabla ya kifo chake, Oktoba 2, 2026 saa tatu usiku, baba mzazi wa mtoto huyo alikwenda kituo cha Polisi Wete kutoa taarifa ya kupotea kwa mtoto huyo. “Imeelezwa kuwa Oktoba 2, mwaka huu mtoto huyo aliondoka saa 12:00 asubuhi kwenda skuli, ambapo hakurudi tena nyumbani kwao mpaka mwili wake ulipoonekana kwenye kichaka akiwa ameshafariki dunia,” alisema. Kamanda huyo alieleza kuwa, mwili wa marehemu huyo ...