TUZ yapokea maoni ya wadau Pemba kuhusu mkataba utoaji huduma
TUME ya Utangazaji Zanzibar TUZ, imeanza kupokea maoni, ili kuimarisha rasimu ya mkataba wa utoaji wa huduma kwa wadau wa habari, ili kujenga ukaribu na uhusiano kwa wadau hao.
Akizungumza
katika kikao cha kupokea maoni ya wadau kuhusu mkataba huo kwa wamiliki wa
vyombo vya habari na wadau wa huduma za
utangazaji, kilichofanyika ukumbi wa
mikutano ZBC Chakechake, Afisa Utawala wa Tume hiyo Zanzibar Zuwena Mohamed alisema,
maoni ya wadau yatasaidia kuwa na rasimu rafiki ya utoaji wa huduma.
Alisema
Tume ya Utangazaji imebaini kuwa, kumekuwepo na baadhi ya watu hawaelewi huduma
zinazotolewa na Tume hiyo, jambo linalopelekea kukosekana kuwepo kwa uhusiano
mzuri kati ya Tume na Wadau.
‘’Tumekua
tukipokea malalamiko mbalimbali kutoka kwa wadau wetu, hivyo tumeamua kuleta
mkataba huu kwenu ili kuutolea maoni ambayo yataingizwa kwenye rasimu hapo
badae yenye lengo la kuondosha malalamiko hayo pamoja na mambo mengine,’’alisema.
Alieleza
kuwa, ujio wa rasimu hiyo ya mkataba huo
wa utoaji wa huduma kwa wataka huduma, utaleta mabadiliko makubwa katika sekta
ya utangazaji, wandishi, wadau pamoja na watendaji wa Tume yenyewe.
Aliendelea
kusema kuwa mkataba huo umegusa vipengele saba muhimu, ambapo moja ni kufanya
mawasiliano na wadau pamoja na kuvitembelea vituo vya utangazaji kila baada ya
miezi sita.
‘’
Vipengele vyengine vilivyomo ndani ya rasimu ya mkataba wa utoaji wa huduma kwa
wadau wa utangazaji ni uwepo wa rufaa kwa mtaka huduma pindi hakupata huduma
kwa wakati,’’alifafanua.
Mapema
akifungua kikao kazi hicho, Mratibu wa Tume hiyo Ofisi ya Pemba Adam Ramadhan
Kombo alisema, lengo hasa la mkataba huo ni kurahisha huduma za utangazaji na
wadauwake katika shughuli zao mbalimbali za utangazaji.
Alieleza
kuwa kwa kujali maoni ya wadau wake, Tume imeona ni vyema kuwakusanya na
kupokea maoni yao, ili kuwa na rasimu rafiki na inayokwenda na wakati.
Hivyo
aliwaomba wadau hao kuendelea kutoa maoni yao juu ya uimarishaji wa rasimu hiyo,
ambayo ni kiungo muhimu baina ya Tume na wataka wataka huduma za Utangazaji.
‘’Hii
ni fursa muhimu kwa wadau wetu, maana chombo hichi ndicho kitakachotuongoza
sisi Tume kufikia malengo ya wataka huduma, ili kutimiza ndoto za shughuli zao
za kila siku,’’alieleza.
Nao baadhi ya wadau walioshiriki kikao hicho, walielezea kufurahishwa kwao, na wazo la Tume ya Utangazaji Zanzibar TUZ, kuileta rasimu hiyo kwao kwani wametekeleza takwa la kisheria.
Mmoja kati ya wadau hao Mustafa Moyo alisema
wakati umefika sasa kwa Tume hiyo kuvifuatilia zaidi vyombo vha habari
mtandaoni hususani TV, ili kuhakikisha vinafuata kikamilifu kanuni za
utangazaji.
‘’Chombo
hichi cha mkataba kitakua suluhisho la wale wamiliki wa vyombo vya habari
wanaokiuka maadili na kufganya kazi pasi na vibali, leseni pamoja na kutofuata
miongozo inayotolewa na TUZ, alieleza.
Nae
Maryam Talib Omar alisema kuwa rasimu hiyo itakapokamilika itakua ni daraja
lenye ufanisi la mawasiliano baina ya Tume na wadau wa Utangazaji, jambo ambalo
kwa sasa sio rafiki.
Tume
ya Utangazaji Zanzibar TUZ kwa sasa inaendelea kukusanya maoni kwa wadau wake,
ili kuwa na mkataba wa utoaji wa huduma kwa wadau wa utangazaji, jambo ambalo
kwa miaka 14 iliyopita halipo.
MWISHO



Comments
Post a Comment