MAGUMU ANAYOYAPITIA MWALIMU WA MADRSA MWENYE ULEMAVU WA VIUNGO PEMBA HAYA HAPA.
Saada Khamis: Mwalimu wa madrassa mwenye ulemeavu Awapatia watoto elimu kwenye mazingira magumu NA FATMA HAMAD, PEMBA ‘’KIPINDI cha mvua wanafunzi hulazimika niwafungie wasije madrasani mpaka zitakapo malizika,’’ hayo ni maneno ya Sada Khamis Hamad mwenye ulemavuwaviungo ni mwalimu wa madrssa. Kwake anasema ulemavu alionao haukua mzigo kuwa asitimize ndota zake za kuwa mwalimu wa madrassa. Hii ni baada ya kuukosa uwalimu wa skuli kutokana na changamoto za hapa na pale, ingawa hakukata tamaa. ‘’Nilikuwa natamani siku moja niwe darasani nafundisha ila sikubahatika, kusoma skuli hata darasa moja, kwani ilikuwa iko maeneo ya mbali na siwezi kutembea,’’anakumbuka. Ukosefu wa kiti mwendo kwa wakati huo, na hasa kutokana na ukata wa fedha waliokuwa nao wazazi wake, ulimkosesha elimu ya skuli. Yote hayo ni masikitiko ya Mwalimu wa Madrasa ya Qur-aan Sada Khamis Hamad mwenye ulemavu wa viungo anaeishi katika kijiji cha Shumba Vyamboni Wilaya ya Micheweni Pemba. M