huduma za maji kuboreshwa vijijini
NA FATMA
HAMAD PEMBA.
Wananchi wa
Vijiji vya Kigongoni, Miongoni pamoja na vijiji vyengine ambavyo havijafikiwa
na huduma ya maji safi na salama wametakiwa
kuwa wastahamilivu kwani wizara husika tayari ipo katika mchakato wa
kumaliza tatizo la upatikana wa huduma
hiyo Vijijini humo.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Maji
Nishati na Madini Zanzibar Shaib
Hassan Kaduara katika ziara yake aliyoifanya Kisiwani Pemba, kwa ajili ya
kuskiliza Kero za Wananchi za upatikanaji wa Huduma ya Maji Safi na Salama.
Amesema
tayari wameshaanza kuyafanyia kazi baadhi ya maeneo na sasa wanaboresha
Miundombinu ili kuona huduma hiyo inapatikana katika vijiji vyote vya Pemba.
‘’Takribani
vijiji vingi ambavyo vilikua na tatizo la ukosefu wa huduma ya maji tayari kama vile Michungwani, Wesha tayari vimeshapatiwa ufumbuzi ‘’ alieleza
waziri.
Wakitoa
changamoto yao mbele ya waziri huyo Wananchi wa michungwani wilaya ya Chake
chake wamesema maji wanayoyapata yamechanganyika na madini chuma kutokana na uchakavu wa miundombinu.
‘’Maji
tunapata japo ni kwa mgao lakini ni machafu
tunashindwa hata kuyanywa kwa
kuhofia afya zetu’’ walisema wananchi wa michungwani.
Mkurungezi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar Zawa Tawi la Pemba, Omar Mshindo
Bakari amewatoa hofu wananchi hao juu ya usalama wa maji hayo.
‘’Kiwango
cha madini chuma kilichomo katika maji hayo hana athari yoyote
hivyo ni waombe wananchi
waendelee kutumia maji hayo
bila wasi wasi wowote’’ alisema mkurugenzi.
Katika Ziara
hiyo waziri Kaduara alitembelea Vianzio
vya maji katika vijiji mbali mbali ikiwemo Kijangwani na Michungwani pamoja na kukagua zoezi la ufikishwaji wa
umeme huko Chokocho Wilaya ya Mkoani Pemba.
Comments
Post a Comment