WANDISHI WA HABARI WAPEWA MBINU ZA KUANDIKA HABARI ZA UDHALILISHAJI.
NA FATMA HAMAD, Wandishi wa habari wametakiwa kufuata madili na miko ya uwandishi wa habari wakati wanapoandika na kuripoti habari zao, ili kuepusha migongano isiyo ya lazima. Akizungumza na wandishi wa vyombo mbali mbali vya habari katika mafunzo ya kuwajengea uwezo jinsi ya kuandika na kuripoti habari za udhalilishaji, Afisa mkuu wa mawasiliano na uchechemuzi kutoka chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania Zanzibar Safia Ngalafi, huko mkanjuni Chake Chake Pemba. Alisema kwa mujibu wa utafiti wa kihabari uliofanywa na Tamwa ili kuona jinsi gani wandishi wa habari wanaripoti habari za udhalilishaji, imeonekana kuwa, bado wandisi hawajakuwa na uwelewa wa kutosha juu ya kuandika na kuripoti habari za udhalilishaji. ‘’ Tulifanya utafiti kwa kuangalia habari zinazoripotiwa na wandishi wa habari kupitia Gazeti la Zanzibar leo, Nipashe, Habari leo, Assalam fm, Furaha, pamoja na soio media.’’ Alisema bi safia. Alisema bado wandishi wa habari wanahitaji