WANDISHI WA HABARI WAPEWA MBINU ZA KUANDIKA HABARI ZA UDHALILISHAJI.
NA FATMA HAMAD,
Wandishi wa
habari wametakiwa kufuata madili na miko ya
uwandishi wa habari wakati wanapoandika na kuripoti habari zao, ili
kuepusha migongano isiyo ya lazima.
Akizungumza
na wandishi wa vyombo mbali mbali vya habari katika mafunzo ya kuwajengea uwezo
jinsi ya kuandika na kuripoti
habari za udhalilishaji, Afisa mkuu wa mawasiliano na uchechemuzi kutoka
chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania Zanzibar Safia Ngalafi, huko mkanjuni Chake Chake Pemba.
Alisema kwa
mujibu wa utafiti wa kihabari uliofanywa
na Tamwa ili kuona jinsi
gani wandishi wa habari wanaripoti
habari za udhalilishaji, imeonekana kuwa,
bado wandisi hawajakuwa na uwelewa wa kutosha juu ya
kuandika na kuripoti habari za udhalilishaji.
‘’ Tulifanya
utafiti kwa kuangalia habari zinazoripotiwa na wandishi wa
habari kupitia Gazeti la Zanzibar leo,
Nipashe, Habari leo, Assalam fm, Furaha,
pamoja na soio media.’’ Alisema bi safia.
Alisema bado
wandishi wa habari wanahitaji kuendelezwa kielimu ili kuona wanandika habari
zenye mashiko na maslahi kwa Taifa na Jamii.
Aidha
aliwataka wandishi wa habari kufanya ufuatiliaji wa stori zao wanazoziandika ili jamii ifahamu
ni kwa namna gani haki imetendeka.
Mapema mkufunzi kutoka chuo cha uwandishi wa habari [Suza] Aiman duwe amewataka wandishi wa habari kujikita zaid kuandika habari za uchunguzi, ambazo zitaleta maendeleo na mabadiloko katika jamii.
Nao wandishi waliopata mafunzo hayo walisema mafunzo hayo yatawasaidia kuandika habari zenye kuleta mabadiliko ndani ya jamii
Comments
Post a Comment