RUSHWA MUHALI BADO NI TATIZO KWA JAMII
NA FATMA HAMAD PEMBA. Imebanika kuwa rushwa muhali bado ni kilio kikubwa kinachoendelea kuikumba jamii hali ambayo inapelekea kesi nyingi za udhalilishaji kufutwa Mahakamani kutokana na kukosa ushahidi. Wakizungumza katika mkutano wa robo mwaka wa kujadili juu ya utekelezaji wa majukumu yao wana mtandao wa kupinga udhalilishaji kutoka wilaya ya Mkoani huko ukumbi wa Chama cha Wandishi wa habari Wanawake Tanzania [Tamwa] iliyopo chake chake Pemba. Wamesema licha ya juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali pamoja na wanaharakati mbali mbali ya kuwafahamisha jamii kufahamu madhara ya udhalilishaji lakini bado juhudi hizo zinagonga mwamba. Wamesema wamebaini kuwa wengi wafanyaji wa matukio hayo huwa ni ndugu wa familia moja, hivyo huzimalizia mitaani hawaendi kutoa ushahidi kwa kuhofia ugomvi katika familia zao. ‘’Sasa hivi kunapotokezea udhalilishaji huamua kupigishana faini wenye kwa wenyewe majumbani hawendi katika vyombo vya sheria kwa k