ANAYEDAIWA KUMLAWITI MTU MWENYE ULEMAVU WA AKILI PEMBA, APATA UZIWI GHAFLA MAHAKAMANI

NA FATMA HAMAD, PEMBA HAKIMU wa mahakama Mkoa Wete, Mwendesha mashtaka, Karani, na askari wa mahakama, wamepigwa na butwaa baada ya baba mzazi wa mtuhumiwa wa ulawiti, kudai mtoto wake ni kiziwi. Awali mtuhumiwa huyo alikuwa ni mzungumzaji mzuri, wakati kesi yake ikiendeshwa mahakamani hapo kabla ya kuondolewa kwa madai ya kudanganya umri. Ilibainika kuwa wazazi wa kijana huyo mwenye miaka 19, anaedaiwa kumlawiti kijana mwenzake mwenye ulemavu wa akili na kisha kupandishwa katika mahakama ya mkoa B Wete, Febuari 13, mwaka huu ingawa kesi yake iliondolewa mwezi Machi mwaka huu baada ya kudaiwa kudanganya umri. Ndipo mahakama ya mkoa ‘B’ ilipompandisha kwenye kizimba chake na kusomewa upya shtaka lake, kama mtu mzima, ingawa baba mzazi kabla ya mtoto wake [mtuhumiwa] kujibu lolote, alidai kuwa ni kiziwi. Hoja ya mzazi huyo, ilichukua takriban dakika mbili mahakamani hapo, ikijadiliwa baina ya hakimu, mwendesha mashtaka na baba mzazi, juu ya ulemavu ulioibuka ghafla na kuwashangaaza waliokuwepo mahakamani hapo. “Mheshimiwa hakimu, mwanangu ni kiziwi ‘hawezi kuzungumza’, hivyo naomba nimsemee juu ya kesi yake , pamoja na masuali yatakayoulizwa mahakamani hapo,’’alidai baba mzazi. Mwendesha mashtaka, kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa mashataka Juma Ali Juma aliingilia kati na kupinga vikali na kuiomba mahakama, isimtambue baba huyo kama wakala wa mtuhumiwa na kutaka mtuhumiwa apelekwe Hospitali kwa ajili ya uchunguzi. ‘’Mheshimiwa hakimu kama mtuhumiwa leo hii ni kiziwa (anaulemavu wa matamshi) basi taratibu zifuatwe kwa mujibu wa sheria, ikiwemo kupelekwa Hospitali kwa ajili ya uchunguzi ili tuendelee na shauri hili,’’ alidai mwendesha mashtaka. Baada ya mabishano hayo, hakimu wa mahakama ya mkoa ‘B’ Wete Ali AbdulI-rahman Ali alikubali na kulighairisha shauri hilo hadi Mei 9, mwaka huu, ili kutoa nafasi kwa mtuhumiwa kupelekwa Hospitali kwa ajili ya uchunguzi ili kubainika ikiwa ni kiziwi ama laa. “Kama mtuhumiwa Kombo Nuhu Kombo ana ulemavu wa matamshi, mahakama haina tatizo na hilo, na wale mashahidi kwanza musiwalete mahakamani, mpaka apelekwe Hospitali na kupata maelezo ya mtaalamu,’alisema Hakimu’. Awali mtuhumiwa huyo, alipandishwa mahakamani hapo akikabiliwa na tuhuma za kumlawiti kijana mwenye ulemavu wa akili, mwenye miaka 19, jambo ambalo ni kosa kisheria. Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, kufanya hyivyo ni kinyume na kifungu cha 116 [1] cha sheria ya Adhabu nambari 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar.

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.