KATIBU MKUU CUF AACHA UJUMBE KWA VIONGOZI WENZAKE
NA FATMA HAMAD PEMBA. Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Hamad Massoud Hamad amewataka viongozi wenzake wa vyama vya siasa nchini kuyaenzi na kuyalinda maridhiano ya Zanzinbar ili kuwafanya watu wote kuwa kitu kimoja. Katibu huyo ametoa wito huo wakati akizungumza na wapenzi na wafuasi wa chama cha CUF katika mkutano wake wa mwanzo tokea kuondolewa kwa zuio la mikutano ya hadhara na Rais wa Jamuhuri ya Muungano Samia Suluhu Hassan huko wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba. Alisema kazi walioifanya viongozi wa Zanzibar akiwemo marehemu maalimu Seif Sharif pamoja na rais mwinyi la kufanya mazungumzo na kuanzisha maridhiano ni jambo kubwa, hivyo niwajibu viongozi kuyaendelenza na kuyatunza maridhiano hayo yaendelee kudumu hapa Nchini. ''Tumekua tukishuhudia kunapomalizika kwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar katika vijiji vyetu hujitokeza migogoro mbalimbali ikiwemo kususiana, hivyo basi Niwasihi viongozi w