KATIBU MKUU CUF AACHA UJUMBE KWA VIONGOZI WENZAKE
NA FATMA HAMAD PEMBA.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Hamad Massoud Hamad amewataka viongozi wenzake wa vyama vya siasa nchini kuyaenzi na kuyalinda maridhiano ya Zanzinbar ili kuwafanya watu wote kuwa kitu kimoja.
Katibu huyo ametoa wito huo wakati akizungumza na wapenzi na wafuasi wa chama cha CUF katika mkutano wake wa mwanzo tokea kuondolewa kwa zuio la mikutano ya hadhara na Rais wa Jamuhuri ya Muungano Samia Suluhu Hassan huko wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Alisema kazi walioifanya viongozi wa Zanzibar akiwemo marehemu maalimu Seif Sharif pamoja na rais mwinyi la kufanya mazungumzo na kuanzisha maridhiano ni jambo kubwa, hivyo niwajibu viongozi kuyaendelenza na kuyatunza maridhiano hayo yaendelee kudumu hapa Nchini.
''Tumekua tukishuhudia kunapomalizika kwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar katika vijiji vyetu hujitokeza migogoro mbalimbali ikiwemo kususiana, hivyo basi Niwasihi viongozi wenzangu tuyaheshimu na tuyatunze maridhiano ili kunusuru migongano hiyo'' alisema katibu mkuu.
Aidha Katibu huyo aliwataka viongozi wenzake wa vyama vya siasa kufanya siasa za kistaarabu jambo ambalo litaepusha kujitokeza kwa vurugu baina ya wafuasi wa vyama tofauti kwenye mikutano yao watakaoifanya.
Kwa upande mwengine mheshimiwa Hamad alisema kitendo cha Rais Samia Suluhu Hassan cha kuruhusu shughuli za mikutano ya hadhara ya kisiasa ni jambo la busara na ni jambo la kushukuriwa.
Akitoa Salamu za wanawake wa Pemba kwenye mkutano huo Bi Fatma Mabrouk amewataka wanachama wanawake kushirikiana katika kukiimarisha chama chao wakitambua kuwa CUF ndo ile ile yenye kujali haki na usawa kwa watu wote.
Mapema Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Mbarouk Seif aliwashukuru wanachama wote waliokuwa nje ya chama hicho na kuamua kurudi ili kuweza kushirikiana na wengine kukiimarisha chama chao.
Katika mkutano huo jumla ya wanachama 513 wa wilaya ya Micheweni kutoka chama cha ACT Wazalendo walichukua kadi za chama cha CUF.
Comments
Post a Comment