MASHEHA WATAKIWA KUTOA ELIMU KWA JAMII KUFAHAMU ULIPAJI WA KODI YA MAJENGO
NA FATMA HAMAD,PEMBA MKURUGENZI wa Bodi ya mapato (ZRA] kisiwani Pemba Jmal Hassan Jamal amewataka Masheha kuielimisha Jamii kufahamu umuhimu wa kulipa kodi ili waweze kulipa kodi jambo ambalo litaipatia Nchi maendeleo. Mkurugenzi huo ameyasema hayo wakati akizungumza na Masheha pamoja na viongozi mbali mbali wa Serikali wa mkoa wa Kaskazini Pemba katika mkutano wa utoaji wa uelewa wa kodi ya majengo huko baraza la Wawakilishi Wete mkoa wa Kaskazini Pemba amesema ulipaji wa kodi ni moja ya chanzo kitakachoipatia Nchi kupiga hatua kimaendeleo. Alisema masheha wana nafasi kubwa katika jamii, hivyo ni jukumu lenu kuwaelimisha wananchi ili kuhakikisha wanatekeleza juku lao la ulipaji wa kodi. ‘’Ndugu zangu masheha ni wajibu wenu kutoa elimu kwa jamii ili kuona wanatekeleza wajibu wa Serikali wa ulipaji wa Kodi,’’alisema. Aidha kwa upande mwengine alifahamisha kuwa miongoni mwa majengo yatakayolipiwa kodi ni majumba ya Ghorofa pamoja na majengo yanayo