WANCHI WA TUMBE WAPEWA USHAURI

                             NA SALIM HAMAD,PEMBA

WANANCHI wametakiwa kutoa mashirikiana kwa  Wasaidizi wa sheria ili waweze kuibua kero zinazowakumba wanajamii na kuweza kutatuliwa.

Hayo yamezungumzwa na Msaidizi wa sharia shehiya ya Tumbe magharibi  Zaina Omar Othman wakati akizungumza na wananchi wa Tumbe  Raha kesho amesema kuna changamoto mbali mbali ambazo zimekuwa zikiwakumba wanajamii  ikiwemo masuala ya Udhalilishaji, na ya ndoa.

Alisema endapo wanajamii watashirikiana na wasaidizi wa sheria kutasaidia kujulikana kwa kadhiya ambazo zimekuwa zikiwakumba wananchi na kuweza kuzisemea, ili kuona mamlaka husika zitakazo lalamikiwa zinachukuwa hatuwa.

‘’Ili kuona tunafikia lengo la kuondosha matatizo katika jamii ni vyema tuwe na mashirikiano ya pamoja baina yetu sisi wasaidizi wa sharia pamoja na wananchi,’’alisema.

Kwa upande wake Msaidizi wa Sheria shehiya  ya Tumbe Mashariki Fatma Hamad ameitaka jamii kuwatumia wasaidizi wa sheria katika kueleza kero zao pamoja na malalamiko yao ili kuona wanapatiwa msada wa kisheria, na kuweza kupata haki zao pindi wakiona viashiria vya uvunjifu wa haki hizo.

 ‘’Kama jamii mutawatumia ipasavyo wasaidiz wa sharia katika kuwaelezea shida zenu, kutaepusha kutokea kwa mogogoro isiyo ya lazima, na kuepuka kupelekana Mahamakamani kwa masuala madoggo madogo,’’alieleza.


Nae msaidizi wa sheria shehiya ya Shumba ya vyamboni Salim Hemed alisema wasaidizi wa sheria wana nafasi kubwa katika kuhakikisha wanatoa elimu juu ya masuala mbali mbali ya kisheria, hivyo ni budi wanachi kitumia fursa hiyo ya wasaidizi hao wa sheria jambo ambalo litawasaidia kupata uwelewa juu ya masuala mbali mbali ya kisheria, pamoja na kufahamu haki zao na wajibu wao kisheria.


Mkutano huo uliandaliwa na jumuiya ya Wasaidizi wa sheria wa wilaya ya Micheweni ( MIDIPAO) ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya utowaji wa elimu kwa jamii kuhusu masuala mbali mbali ya  kimaendeleo.



Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.