umasikini wapelekea Vilabu kushindwa kusaili na uhamisho wa wachezaji Kisiwani Pemba
SALIM HAMAD,PEMBA UKATA wa Kifedha unaovikabili Vilabu vya Madaraja mbali mbali Kisiwani Pemba,umesababisha Dirisha la usajili na uhamisho wa wachezaji kusuasua kutokana na baadhi ya Vilabu kushindwa kujitokeza katika Ofisi za Shirikisho la Soka (ZFF) Kisiwani hapa. Dirisha la Usajili na Uhamisho Visiwani Zanzibar limefunguliwa rasmi Septemba 21 ambapo litarajiwa kufungwa Novemba 11. Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Katib Msadizi wa Shirikisho la Soka Kisiwani Pemba,Khamisi Hamad Juma alisema Zoezi la Usajili na uhamisho limekuwa gumu msimu huu kutokana na baadhi ya Vilabu kushindwa kuchukua fomu. Alisema moja ya sababu inayopelekea vilabu kutojitokeza kuchuka fomu za Usajili na wachezaji wanatka kuwasajili ni kutokana na ukata wa kifedha unaovikabili vilabu vya Pemba,jambo ambalo limepelekea zoezi hilo kusuasua. Alisema hadi sasa timu zilizojitokeza kuchuwa fomu kwa upande wa Primia ni timu ya Machomane United ambayo imechukua fomu 7 na timu ya Yoso Boys imechukua