KIJANA MOHD HAMAD WA KENGEJA MKOANI PEMBA BADO AENDELEA KUSOTA RUMANDE KWA TUHUMA ZA UBAKAJI
Kutokuwepo
kwa Shahidi ambae ni askari mpelelezi kumemlazimu Hakimu wa mahakama ya Mkoa
B’’ Lusiano Makoe Nyengo kughairisha kesi ya kuingilia kinyume na maumbile
ambayo inamkabili mtuhumiwa Ayoub Mohd
Hamad mwenye umri wa miaka 18 mkaazi wa Kengeja Wilaya ya mkoani Pemba.
Baada ya
mtuhumiwa huyo kupanda kizimbani wakili
wa Serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka [DPP] Ali Amour Makame amesema shauri hilo lipo kwa
ajili ya kusikilizwa na leo tulikua
tunashahidi mmoja tu ambae ni askari mpelelezi ila hayupo mahakamani hapa.
‘’Mheshimiwa
leo tulikua tunashahidi askari mpelelezi ila hayupo kwani yupo mafunzoni, hivyo
tunaiomba mahakama yako uipangie tena siku nyengine kwa ajili ya kusikilizwa’’,
Alisema DPP.
Kwa upande
wake Wakili mtetezi anaesimamia kesi
hiyo Zahrani Yussuf hakukubaliana na maelezo hayo yaliotolewa na wakili wa
Serikali, kwamba shahidi hapatikani, hivyo ameiomba mahakama itoe oda
kwa kuzingatia haki ya mshitakiwa kwani ameshakaa rumande
kwa muda mrefu.
‘’Mheshimiwa
tunaomba mahakama yako itoe oda, na
lazima tuangalie pande zote mbili, hivyo
tukiendelea tuu shahidi hapatikani
tunamuumiza mtuhumiwa, Alisema wakili mtetez’’.
Hakimu wa
mahakama hiyo Lusiano Makoe Nyengo hakukubaliana na ombi la wakili mtetezi na
kesi itaendelea tena tarehe 14/9/mwaka huu. Imedaiwa kuwa mtuhumiwa huyo
alitenda kosa hilo siku ya tarehe 23/2/2021 majira ya 5;30 asubuhi, huko Likoni
Kengeja wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba Alimuingilia kinyume na maumbile
ambapo kufanya hivyo ni kosa kinyume na kifu cha 133 [a] cha sheria ya adhabu
sheria nambari 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar.
Comments
Post a Comment