TATIZO LA MAJI LILILOKUWA LINAIKABILI KITUO CHA AFYA WESHA SASA LAPATA UFUMBUZI
NA FATMA HAMAD, PEMBA Septemba 21 mwaka huu Blog ya Pemba ya leo iliibua changamoto ya kukosekana kwa huduma ya Maji safi na salama katika kituo cha Afya cha Wesha wilaya ya Chake chake Pemba, ambapo kilio hicho kimepatiwa ufumbuzi kwa sasa. Wakizungumza na mwandishi wa habari huko kituo cha afya wesha Safinia Said na Rukia Khamis ambao ni wajawazito waliokwenda kupata huduma kituoni hapo walisema zaid ya miezi 3 kulikuwa hakuna maji kituoni hapo. Walisema kwa sasa shida ya Maji imepungua kwani Maji yanapatikana ijapokuwa hayatoki siku zote ni kwa mgao. ''kwa sasa hatuendi na madumu ya Maji tunapokwenda kujifungua kwani Maji ya zawa ikifika zamu ya kutoka huwa yanapatikana hapa kituoni,, walisema Hivyo tunaiomba Wizara ya Maji iyongeze juhudi ili kuona Maji yanapatikana masa yote 24 kwani suala la uzazi ni kitu cha kila siku jambo ambalo litaondosha usumbufu kwa mama wajawazito pamoja na wazazi wanaokwenda kujifungulia kituoni hapo. Kwa u