BARAZA LA USHINDANI HALALI WA BIASHARA MUARUBAINI KWA WADAU WA BIASHARA



NA FATMA HAMAD, PEMBA
Afisa  Mdhamini wizara ya Biashara na Viwanda kisiwani Pemba Ali Suleiman Abeid amewataka wadau wa biashara kuitumia fursa ya kupata huduma katika Baraza la Ushindani Halali wa Biashara ili waweze kupata majibu sahihi  na  kwa wakati muafaka dhidi ya mashauri yao mbali mbali yanayohusiana na biashara.

Afisa huyo ameyasema hayo wakati akifunguwa kongamano la kuwajengea uwelewa Masheha wa Chake chake na Mafisa Wandamizi wa Mamlaka za Udhibiti kulifahamu baraza la ushindani halali wa Biashara huko Tibirinzi kisiwani Pemba.

Amesema uwepo wa Baraza hilo la Ushindani halali wa Biashara kunakisi azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar juu ya dhamira yake ya kuweka mfumo thabiti wa kusimamia na kuimarisha mazingira  rafiki ya biashara na uwekezaji Nchini.

Alisema  ni vyema Masheha kuwaelimisha wadau wa biashara  pamoja na watumiaji ili wawe na ulewa wa hali ya juu na kuona wanalitumia Baraza hilo pale ambapo hawakuridhika na mamuzi yaliyotolewa na Mamlaka za udhibiti.

 ‘’Nyinyi Masheha mnanafasi kubwa katika Jamii hivyo ni vyema kutoa Elimu kwa Wafanyabiashara na watumiaji ili kuona wanalitumia Baraza hilo kwa kupeleka kero zao,’’ alisema.

Akiwasilisha mada kuhusu sheria  namba 5 ya mwaka 2018 ya ushindani na kulinda mtumiaji Mrajisi wa Baraza la Ushindani halali wa Biashara Fatma Gharib Haji alisema lengo la kuwepo kwa baraza hilo ni kuzuia vitendo vinavyokwenda kinyume na ushindani wa biashara na visivyokubalika katika biashara.


Kwa upande wake Mwanasheria wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Pemba Suleiman Khalfan alisema kuwepo kwa Baraza hilo kutawasaidia Wafanya biashara pamoja na watumiaji kupeleka malalamiko yao pamoja  na changamoto zinazowakwanza na kuweza kutatuliwa.

Aidha amewataka Viongozi wa Baraza hilo kuendelea kutoa Elimu kwa watu mbali mbali ili waweze kulifahamu na kulitumia, kama ilivyo dhamira ya Serikali la kuondosha changamoto za wafanya biashara pamoja na watumiaji biashara.

Nao baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wameushukuru Uongozi wa baraza Halali la Ushindani wa Biashara kwa kuwapatia elimu hiyo, hivyo wameahidi kuifanyia kazi ili kuona wafanyabiashara wanafanya biashara zao kwa mujibu wa sheria namba 5 ya mwaka 2018 kama ilivyoelekeza.




Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.