KIRARE BADO AISOTEA RUMANDE
FATMA HAMAD PEMBA. Mahakama ya mkoa B iliopo Kusini Pemba imeghairisha kesi ya kuingilia kinyume na maumbile inayomkabili kijana Khamis Abdala Khamis marufu kirare mwenye umri wa [20] mkaazi wa Kangani wilaya ya Mkoani baada ya mtuhumiwa huyo kukataa kusomewa shitaka lake . Kijana huyo wakati akiwa ametulia kizimbani na kusubiri asomewe shitaka lake aliambia mahakama hiyo kuwa hali yake sio mzuri anaomba kesi ighairishwe na ipangiwe siku nyengine. ‘’Mheshimiwa hakimu leo naumwa siwezi kukakaa hivyo naiomba mahakama yako ighairishe shauri hilo kwa leo’’ alieleza mtuhumiwa kirare. Hakimu wa mahakama hiyo Muumin Ali Juma amesema hii ni mara ya pili unasema unaumwa daktari anakuja na kurudi ila ujue baadae fursa hii hutoipata tena nitakua sikusikilizi tena , na mahakama itatoa oda ya kumruhusu daktari afanye shughuli zake mpaka utakapo kuwa tayari ndio tutamleta na wewe utarudi rumande hadi tarehe 9/ 8 2022kwa ajili ya kusikiliza mashahidi. Mtuhumiwa h