AFUNGWA JELA KWA KUTOROSHA MSICHANA

 



NA FATMA HAMAD PEMBA.

Hatimae kijana  Ramadhan Khamis Mohd  mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa Tironi  Mkoani Pemba  anza  maisha  mapya  ya kutumikia chuo cha Mafunzo kwa muda  wa miaka 5 baada ya kutiwa  hatiani  kwa kosa  la  kutorosha  msichana  wa  miaka  16.

Baada ya kijana huyo kupanda kizimbani na kusubiri asomewe hukumu yake Mwendesha mashtaka  wa Serikali Mussa Khamis amemuambia  hakimu anaendesha kesi hiyo kuwa kesi iko kwa ajili ya kutolewa uwamuzi hivyo wao hawana pingamizi kama mtuhumiwa yuko tayari basi asomewe huku yake.

‘’Kama mtuhumiwa yuko tayari basi na sisi hatuna tatizo nivyema  asomewe hukumu yake ili ajue hatma yake’’ alieleza  DPP Mussa.

Hakimu wa mahakama ya mkoa B  iliyopo Chake chake  Muumin  Ali Juma   alisema jumla ya mashahidi 4 walisikilizwa mahakamani hapo akiwemo muathirika mwenyewe na Mahakama imemtia hatiani mtuhumiwa huyo.

Hivyo kwa mujibu wa kifungu cha 113 [1] [a] cha sharia ya adhabu namba  6  na  kifungu  cha  299  cha sharia  ya mwenendo wa makosa ya jinai sharia namba 7 za mwaka 2018 sheria za Zanzibar  kijana huyo atatumikia  chuo  cha  Mafunzo  kwa  muda  wa  miaka  5.

Imedaiwa mahakamani hapo siku ya tarehe  16/1/ 2021  majira ya saa 1;30 za usiku  huko  Tironi wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba Kijana huyo  bila ya halali na bila ya ridhaa  ya wazazi wake  alimtorosha   msichana wa miaka 16 kutoka nyumbani kwao na kumpeleka  katika  geto la Yakuob  Abdala  Juma  hapo  hapo  tironi  jambo  ambalo  ni kosa  kisheria.

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.