Posts

Showing posts from July, 2026

ADAIWA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA MIWILI

Image
NA FATMA HAMAD, PEMBA KIJANA SHAAME Ali Hamad anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka (38) mkaazi wa Mchangamdogo wilaya ya Wete Pemba, ashikiliwa na adaiwa za kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka miwili na miezi mitatu. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko nyumbani kwake, mama wa mtoto huyo alisema mtoto wake alifanyiwa tukio hilo la kinyama akiwa nyumbani kwa jirani yake ambae ni mtuhumiwa. Alisema, siku ya Ijumaa ya tarehe 26/06/2026 akiwa nyumbani kwake akifanya shughuli zake, mtoto wake alikuwa hajamuona muda mrefu, ndipo aliponza kumtafuta na kumuita kwa jina ingawa hakubahatika kumuona kwa wakati huo. ‘’Nilirudi nyumbani kuendelea kufua lakini nilifanya wasiwasi na nikaamua kwenda kumtafuta tena, ndipo nikamkuta amekaa nje ya mlango wa nyumba ya Shaame, akiwa na hali ya huzuni,’’ alisema. Alisema, alimwambia asimame ili waondoke lakini mtoto huyo hakuweza kusimama na akambeba na kwenda nyumbani kwao na kumueka huku yeye akiendelea na shughuli zake. Alisema, baada ya ...