NA FATMA HAMAD, PEMBA
Wakati taifa likijivunia ongezeko la wanawake katika
nafasi za maamuzi, changamoto ya udhalilishaji wa kijinsia inaendelea kuwa
kikwazo kinachowakatisha tamaa wanawake wengi kuingia katika siasa na uongozi.
Matusi ya mitandaoni, kejeli zinazolenga mwonekano, vitisho,
lugha ya kudhalilisha na propaganda zinazolenga jinsia badala ya uwezo wa
kiongozi zinaendelea kushamiri.
Licha ya kwamba hata Raisi wa Tanzania ni mwanamke bado
wapo baadhi ya wanajamii wamekua na mitazamo tofauti dhidi ya viongozi
wanawake kwa kutokana na jinsia zao.
Wadau wa haki za binadamu wanaonya kuwa idadi halisi inaweza
kuwa kubwa zaidi kwa sababu matukio mengi hayaripotiwi kutokana na hofu, aibu
au mila zinazowazuia waathirika kuzungumza.
WENYEWE VIONGOZI WANAWAKE WANASEMAJE JUU YA HILI
Mkufu
Faki Ali ni Katibu tawala wilaya ya Wete Kaskazini Pemba anasema maranyingi
vikwazo vinavyomkwaza katika uongozi wake ni nidharau nakuitwa maneno mabaya.
Anasema
wapo baadhi ya wanajamii wanaona hawawezi kuongozwa na mwanamke, na maranyingi
hata inapotokea jambo ukalikemea ama ukawaelekeza jambo lenye maslahi nao,
lakini huonekana kama msumbufu tu.
‘‘Wapo
baadhi ya watu hunidharau na hunipa maneno yanye kukatisha tama, nambiwa hasa
huyu bibi kashazeeka kwanini hakai nyumbani kwake akalea wakuu zake anatusumbua
tu,’’anasema.
Anasema
muda mwengine hufanyiwa udhalilishaji katika mitandao ya kijamii, mfano Rais wa
mungano Samia Suluhu Hassan amekua akichorwa vikatuni, jambo ambalo
linawadhalilisha na kuwatia hofu viongozi wote wanawake, kuzungumza na wananchi
wao baadhi ya mambo.
Sheha
wa Njuguni Wingwi wilaya ya Micheweni, Hadia Omar Dadi anasema kikwazo
kikubwa anachokipitia ni kupewa matusi na maneno ya dharau, kutoka kwa
baadha ya wananchi wake.
‘’Tunaambiwa
toka lini mwanamke kuwa kiongozi, na kuna baadhi ya mambo wanaume hukaa kikao
msikitini na kuamua jambo mfano watoto wasiende tv usiku basi mimi , kama sheha
si shirikishwi, hiyo ni dharau.
Anasema
kikwazo chengine kinacho mkwaza ni kukosa usafiri wa kufika katika baaadhi ya
maeneo hususani wakati wa usiku.
‘’inaweza
kukatokea tatizo usiku unapigiwa simu ufike, igawa inakua ni shida, Napata hofu
kufika kwenye tukio hasa mida hiyo ya usik,’’anasema.
Nasra
Ali Salim ambae alikua Diwani zaidi ya awamu 10 anasema kikwazo kikubwa
ambacho huwakumba viongozi wanawake ni dhana mbaya kwamba ukiwa kiongozi
unakua muhuni.
‘’Mwanamke
yule yule anakwenda shamba, anakwenda mwani peke yake wala hatiliwi shaka, ila
ukipata nafasi ya uongozi tu utaambiwa unakwenda kuvuja maadili yako,’’
anasema.
WANANCHI
Zeyana
Seif Nassor kutoka Pandani Wete Kaskazini Pemba anasema watu huwadharau
viongozi wanawake kwa kutokana nan a jinsia zao, wanahisi hawezi kuongoza.
‘’Ni
baadhi tu ya watu hususani wanaume wanahisi mwanamke si kiongozi, na wala
hawamini kuongozwa na wanawake,’’ anasema.
Anasema
suala la uongozi lianze kufundishwa kuanzia ngazi ya familia, ili kuondosha
mitazamo potofu juu ya uongzi kwa mwanamke.
Omar
Khamis mkaazi wa Wingwi wilaya ya Micheweni Kaskazini Pemba anasema suala la
uongozi lifundishwe kuanzia ngazi ya familia, watu wafahamu na waondokane na
mifumo dume na kua na imani juu ya kiongozi mwanamke.
WANAHARAKATI
Mkitu
Hassan Mwalim mwanaharakati wa masuala ya wanawake na watoto kutoka Wingwi
anasem katika Jamii bado wapo watu huwadharau na kushambulia kwa matusi
viongozi wanawake, kwani wanahisi anaefaa kuongoza ni mwanamme tu.
‘’bado
viongozi wanawake wanadharauliwa ni hilo ni kutokana na hali zao na jinsiq y,’’anasema.
Asya Hakim Makame Afisa kutoka Chama cha
Wandishi Habari Wanawake Tanzania TAMWA Zanzibar anasema kwa sasa wanatekeleza
mradi wa "Tunaweza Pamoja" kwa ushirikiano wa UN Women.
Mradi huo unafadhiliwa na serikali ya Norway chini ya mpango wa
Umoja wa Mataifa unaolenga kujenga jamii salama dhidi ya vitendo vya
udhalilishaji kwa wanawake na wasichana.
Ikiwa Mradi
huo wa Tunaweza pamoja unatekelezwa katika Mikoa ya Kaskazini mwa Pemba na
Unguja, ambao lengo lake ni kuondosha vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake na
wasichana
VIONGOZI WA SERIKALI
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, maranyingi
anasisitiza kuwa wanawake wanapaswa kuthaminiwa kwa uwezo wao wa kuongoza
badala ya kuhukumiwa kwa jinsia yao.
Mara
kadhaa amekemea lugha za matusi na udhalilishaji dhidi ya wanawake katika
siasa.
Spika
wa zamani wa Bunge, Anne Makinda, aliwahi kueleza kuwa wanawake wanaoingia
kwenye uongozi hukutana na vikwazo vikubwa kuliko wanaume, ikiwemo matusi,
kejeli na mashambulizi ya maneno yanayolenga kuwakatisha tamaa.
Aliyekuwa
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha-Rose Migiro, amesisitiza mara
kwa mara umuhimu wa kuwawezesha wanawake kushiriki katika maamuzi bila hofu ya
ubaguzi au udhalilishaji.
VIONGOZI WA DINI
Sheikh
Said Ahmed Mohamed, kutoka Ofisi ya Mufti Pemba, anasema dini imempa nafasi
mwanamke ya kushika nafasi yoyote ya uongozi, ilimradi asivunje miiko na
maadili ya Taifa lake.
Yohana
Ali Mfundo ambae ni Mchungaji kutoka Kanisa la Mkusanyiko wa Mungu Tanzania
(TAG) lililopo Ngerengere Chake Chake anasema, dini yao haijambagua mwanamke
asiwe kiongozi, ispokua aendeshe kwa kufuata taratibu na sheria zinavyoelekeza.
ZAECA
Kamanda
wa kudhibiti na kupambana na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) mkoa wa Kusini
Pemba Mustafa Hassan Issa anasema wao hawapokei malalamiko ya udhalilishaji,
isipokua ni kwa kesi za rushwa.
MIKATABA
Kwa
mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na tafiti za afya na maendeleo ya
jamii, wanawake wengi nchini bado hukumbana na aina mbalimbali za ukatili wa
kijinsia, ikiwemo ukatili wa kimwili, kingono na kisaikolojia wa mwaka 2022 .
Takwimu
hizi zinaonesha kuwa ukatili dhidi ya wanawake bado ni changamoto ya maendeleo.
Tanzania
inaendelea kupiga hatua katika kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za
maamuzi, Hata hivyo, ongezeko la uwakilishi halijaondoa changamoto ya
udhalilishaji wa kijinsia.
Mara
nyingi viongozi wanawake hukumbana na mashambulizi yanayolenga utu wao badala
ya hoja zao.
Kwa
mujibu wa Serikali ya Tanzania, wanawake wanawakilisha zaidi ya asilimia 36 ya
wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na takribani asilimia 40 ya wajumbe wa
Baraza la Wawakilishi Zanzibar, hatua inayoonyesha maendeleo katika ushiriki wa
kisiasa kuanzia 2020-2025.
Kwa
upande wa takwimu za ukatili wa kijinsia, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali
Zanzibar imekuwa ikitoa taarifa za kila mwezi.
Takwimu
kutoka Ofisi ya Mtakwimu wa Serikali kwa mwaka 2024 jumla ya matukio 1,809 ya
ukatili wa kijinsia yameripotiwa, visiwani Zanzibar.
kwa
mujibu wa Utafiti wa Viashiria vya Demografia na Afya nchini Tanzania
(Tanzania Demographic and Health Survey - TDHS) Aidha, wanawake
takribani asilimia 14 Zanzibar wamewahi kupitia ukatili wa kimwili, huku karibu
mwanamke mmoja kati ya kumi akiripoti kufanyiwa ukatili wa kingono.
Alisema Takwimu kutoka Ofisi ya Mtakuimu mkuu wa serikali ya
Zanziba Machi 2026 kuliripotiwa matukio 103 ya ukatili na udhalilishaji, ambapo
watoto ilikua ni 84 sawa na asilimia 81.6 wanawake wakiwa ni 17 sawa na
asilimia 16.5.
Utafiti
uliofanywa na Taasisi ya Women at Web kwa kushirikiana na Tamwa Tanzania hivi
karibuni asilimia 79 wanawake wanasiasa na wanaharakati wa kisiasa, walifanyiwa
ukatili wa kijinsia walifanyiwa ukatili wa kijinsia kwa njia ya mtandao katika
uchaguzi mkuu wa 2020.
CHANZO MWANANCHI.
Hotuba ya
Waziri wa nchi - 0fisi ya Rais - Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala bora
Mheshimiwa DKT Haroun Ali Suleiman imeweza kushirikiana na taasisi mbali mbali
katika kupambana na kupunguza kesi za udhalilishaji kutoka kesi 348 kwa mwaka
2023/2024 hadi kesi 292 kwa mwaka 2024/2025.
Katika miaka ya hivi karibuni, China imekuwa ikihimiza maendeleo ya sifa bora ya mambo ya wanawake nchini humu, siku zote inafanya juhudi za kujenga mazingira ya kimataifa yanayosaidia maendeleo ya wanawake, na kutoa mchango muhimu kwa ajili ya mambo ya wanawake duniani.
MWISHO.
Comments
Post a Comment