NAJIVUNIA KUONA WANANCHI WA MJINI KIUYU WAKIKANYAGA BARABARA YA LAMI
NA FATMA HAMAD, PEMBA
‘’Ama kweli mwenye kutafuta haachi kupata’’
Msemo huo
umesadilifu kwa Nassra Salim Mohamed Diwani mstaaf wa wadi ya Kiuyu Minungwini wilaya ya
Wete mkoa wa Kaskazini Pemba.
MAISHA YA
NASRA
Baada ya
kuzaliwa 1969, Nasra alianza kuisaka
haki ya elimu ya msingi mwaka 1976 katika skuli ya msingi Piki wilaya Wete.
Akiwa
darasani, Nasra hakuwa mtulivu na jinsia yake ya kike, wakati mwengine
aliisahau kwa kule kujichanganya na wanafunzi wa kiume kwa ujasiri wa kutafuta
elimu.
Ndio maana
kwenye darsa alilosoma lililokua na wanafuzni zaidi ya 80 waalimu wake hawakurudi nyuma na kumpa
uongozi wa darasa.
Akiwa
nyumbani kwake Kiuyu Minungwini na kujikunjulia utaji wa Kanga za kisutu,
anasema uongozi wake ulipendwa na walimu.
‘’Pamoja na
ufupi wangu na jinsia yangu ya kike, walimu waliniamini kunipa uongozi kuanzia
darasa la kwanza hadi darasa la sita kwa wakati huo nilipofanya mtihani,’’anaeleza.
Ingawa kwa
Nasra kuongoza wanafinzi 80 hakujua kua ni sehemu ya uongozi wala haikua
matayarisho yake ya kushika hatamu ya uongozi, kama ilivyopita miaka 10 nyuma.
Miaka
Arubaini iliyopita wakati akimaliza darasa la Kumi na moja kama elimu ya lazima
kwa wakati huo, Nasra aliendelea kua kiongozi.
Anakumbuka
vyema kuanzia darasa la Tisa, huku akili ya kitoto ikiwa ameshaiaga hamu ya
kuongoza sasa imetawala kwenye akili yake.
‘’Hata
nikirudi skuli ndugu na kaka zangu sikuacha kuwaongoza kwa baadhi ya mambo,’’
anaeleza Nasra.
Nasra
aliyezaliwa miaka 57 iliyopita kijijini kwao Tondooni shehia ya Kisiwani kwa Binti
Abedi iliyomo wilaya ya Wete, alikolea zaidi uongozi baada ya kumaliza masomo.
Akiwa
nyumbani kwao suala la kutegemea wazazi kila kitu kwake lilikua mwiko, kuanzia
mwaka 1990 alijiunga Chuo cha Ufundi JKU, ili awe mtaalamu wa kuzishona nguo.
‘’Lengo la
kujiunga na Chuo cha ufundi kwanza ni kupata ukakamavu, ufundi wa kuzishona
nguo kwa lengo la kuanza kujitegemea kama mtoto wa kike,’’ anasimulia.
Diwani huyo
mstaafu baada ya kumaliza harakati za ufundi JKU, alirudi mtaani na kuanza
kukushanya shilingi moja moja zilizotokana na kusukuma ringi ya Charahani kwa
kuviunga vipande vya vitambaa na kuwa nguo yenye kuvalika.
Nasra
alishazaliwa, mwaka 1969 la pili la mwanadamu la kufunga ndoa, ambapo mwaka 1993
nae alipata wa kumtunza huku akiwa fundi mtaalamu wa ushonaji wa nguo
mbalimbali.
‘’Wakati
nafunga ndoa Nasra nimeshanza kujitegemea na kuwa na uhakika wa kupata visenti
kwa ajili yangu, mume wangu, wazazi na ndugu wa karibu,’’anasema.
NASRA NA
UJASIRIAMALI BAADA YA NDOA.
Akili, Fikra, mawazo na ndoto za Diwani huyu mstaafu kujua kwake
kushona kumbe haikua mwisho wa kusaka visenti.
Ndio maana miaka 16 akiwa katika ndoa alijiunga na ujasiriamali
wa utengenezaji wa mikoba ya ukili, katika kikundi cha Vuta heri.
‘’Kwasasa kikundi hicho kimebatizwa jina na kuitwa ‘’Nguvu yetu
ni umoja’’kilichopo Kiuyu Minungwini wilaya ya Wete tukijishughulisha na
utengenezaji wa sabuni za mwani, mafuta ya Mkaratusi na mapambo ya
harusi,’’anasema.
Baada ya kuingia kwenye ushirika huo ujasiri, hekma na mbinu za
kuwashirikisha wenzake uliwavutia na kumpa nafasi ya uratibu.
Kuanzai mwaka 2008 na miaka minne mbele Chama cha wandishi wa
Habari wanawake Tanzania TAMWA Zanzibar ilitua kisiwani Pemba na mradi wa
kuwawezesha wanawake kiuchumi, na Nasra akawa Mkufunzi.
Ndani ya uendeshaji wa Mradi huo Nasra alijifunza mambo kadhaa
hasa ya uongozi, na namna ya utatuzi wa mogogoro, jambo lililompa nia ya kutaka
nafasi zaidi za uongozi.
NASRA
NA UONGOZI NJE YA ASASI
Hamu ya kutaka kuongoza wanakiuyu Minungwini ilianza kugagaa
ndani ya akili yake mwishoni mwa mwaka 2014 alipoitangazia nafsi yake kuutaka
Udiwani wa wadi ya Kiuyu.
Ndio maana mwaka 2015 haikua tu kwa wagombea Uraisi, Ubunge, na
Uwakilishi bali hata Nasra Mohamed Salim nae alichukua fomu kutafuta ridhaa ya
wananchi.
Harakati za kuchukua na kurejesha na kisha kampeni zilianza kwa
mwanamke huyu shupavu, akishindana na wagombea wa zaidi ya vyama tisa woote
wakiitaka wadi ya Kiuyu Minungwini.
Mwishoni mwa Octoba mwaka 2015 haikua siku tu ya furaha kwa
walioshinda viti vya Uraisi pekee, hata Nasra Mohamed Salim alitokwa na machozi
ya furaha baada ya waliommiminia kura kutaangazwa kuwa Diwani.
Kiongozi huyo wa Wadi ya Kiuyu minungwini kwa wakati huo, nahasa
baada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi makundi ya wanaCCM wenzake yalivunjika na kua kitu kimoja na sasa
ikawa nguvu zote ni kuvitanata vijiji vya wadi ya Kiuyu kimaendeleo.
‘’Nilipokua nagombea nafasi hii nakumbuka nilitoa ahadi
mbalimbali, ikiwemo ujenzi wa Barabara kutoka Penjewani hadi Mjini Kiuyu, ili
kuwapunguzia dhiki wapiga kura,’’anaeleza.
Anakumbuka vyema wakati akiwa Diwani siku aliyosimamishwa mbele
ya Wananchi akiwepo Rais wa Zanzibar ndani ya Jimbola Kojani, alipotakiwa
kuainisha changamoto zinzowakabili na kufanya hivyo bila ya kutetemeka.
‘’Kwakweli siku aliyokuja Rais wa Zanzibar na kusimamishwa
ghafla nilikua mzito kuanzia miguu hadi
mikono, ingawa baada ya kufika kwenye kisemeo,(maiki) nilitiririka mithili ya
maji yaliyokua mlimani,’’anaeleza.
Hawa kukosea wahenga waliosema kuwa mramba asali harambi mara
moja, msemo huu umesadif kwa Diwani Nasra kwa kule wananchi kumrejesha tena
nafasi hiyo mwaka 2020.
Mwenyewe anasema kuwa kuanzia mwezi wa tano 2020 wapo wanachama hatanje
ya chama cha Mapinduzi waliomtaka kuchukua tena fomu ya Udiwani.
‘’Inawezekana ujasiri wangu utekelezaji wa ahadi na ushirikiano
kwa wananchi wote ndio yaliyowasukuma hao wanachama kuniomba kuingia
tena,’’anaeleza.
Kumbe kwa miongo zaid ya mitano Wadi ya Kiuyu haikua na barabara
hata ya kifusi au shule ya kisasa, ingawa kelele za Diwani huyo ziliishawishi
serikali kuu kutekeleza miradi mikubwa ikiwemo uimarishaji wa huduma za Afya.
Ndani ya miaka kumi enzi za Diwani huyo vipo vikundi 25
vilivyotengenezewa mazingira ya kujisajili na kutambulika rasmi, jambo
lililoshindikana kwa miongo iliyopita.
USHUHUDA
WA WANANCHI
Mbarouk
Salim kaazi wa Mjini Kiyu anasema kabla ya ujenzi wa barabara hiyo, magari yalikuwa hayawezi kufika katika maeneo yao
hasa kipindi cha mvua.
‘’Tulikua tukipata mgonjwa hasa wakati wa usiku hatukijua tumfanye nini, kutokana nan a kukosa usafiri’, anasema.
Fatma Khalfan mkaazi wa Kiuyu Penjewani, anasema wagonjwa na wazazi walikuwa wakipata mateso wakati wa kusafirishwa kwenda hospitali.
‘’Siku moja mtoto wa jirani yangu alijifungulia njiani wakati alipo akipelekwa Hospitali, kutokana na ubovu wa barabara,’’anasema.
Hamad Said Hamad miaka (70) ‘’Belfu’’ kutoka Tuliani anasema zamani wagonjwa wakiwabeba kwa vitanda hadi kufika barabara kuu, hali iliyotoa mwanya baadhi ya wagojwa pamoja na wajawazito kutibiwa majumbani.
‘’Wagonjwa tulikua tunawabeba kwa kitanda, tukaona hilo ni tatizo, tuliandika barua tukapeleka kwa Nasra, hakudharau siku ya pili alikuja na timu nzima ya serikali shehia na ya jimbo, tukajengewa njia hii,’’anasimulia.
VIONGOZI WA SERIKALI
Katibu Tawala wilaya Wete, Mkufu Faki Ali, anasema maendeleo ya barabara hizo yamechangia kuboresha huduma za kijamii na shughuli za
kiuchumi.
‘’Barabara hizi zinasaidia wananchi wa vijiji hivyo,
wameondokana
na shida ya usafiri ,’’ anasema.
Naibu sheha Shehia ya Kiuyu Minungwini Haji Kombo Hamad anasema jumla ya wananchi 2682 wa Mjini kiuyu walikua na changamoto ya barabara hio zaidi ya mika 30.
‘’Maendeleo na uchumi wa wananchi umekua, wanasafirisha biashara zao na wanafikia huduma wanazozihitaji kwa wakati, mfano Hospitalini,’anaeleza.
Diwani wa sasa wa Wadi hiyo ya Kiuyu Minungwini Hassan Khamis Hamad anasema kuwa ushiriki wa wanawake katika nafasi za maamuzi, unaendelea kuonyesha uwezo sawa kati ya wanawake na wanaume, katika kusimamia maendeleo.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum wa serikali ya Jamuhuri ya Mungano Mwanaidi Ali Khamis, anasema Tanzania inaendelea kutambua umuhimu wa Wanawake kwa kuwapatia fursa katika nafasi za Uongozi na Maamuzi.
Anasema
mabadiliko hayo yanatokana na dhamira ya Rais wa Jamuhuri ya Mungano Dkt Samia
Suluhu Hassan, ya kuhakikisha usawa kati
ya Wanaume na Wanawake, katika nyanja zote.
"Serikali
inaendelea kusimamia utekelezaji wa mikataba ya Kikanda na Kimataifa inayolenga
kukuza Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji Wanawake hapa nchini,’’anamalizia.
WANAHARAKATI
Mkufunzi kutoka Chuo cha Taifa Zanzibar (SUZA) Aimane Othman Duwe anasema wanawake wanapopewa nafasi za uongozi huleta mabadiliko, hutatua changamoto za jamii, hususan zinazohusu huduma za msingi kama afya.
‘’ Mwanamke ni mama, ni mtu ambae maranyingi hua karibu na jamii,anajua shida zinazowakabili, hivyo anapopata nafasi ni rahisi kuleta mabadiliko,’’anasema
Afisa Programu wa masuala ya wanawake na uongozi kutoka Chama cha Wandishi wa Habari Wanawake TAMWA Zanzibar Khairat Ali anasema mchango wao wanaoufanya ni kutoa elimu na kuhamasisha wanawake wapewe nafasi za maamuzi.
‘’Mwanamke ni mama, na maranyingi mama hupenda afanye mazuri ili mtoto wake abaki salama,’’anasema.
USHUHUDA WA VIONGOZI WANAWAKE WALIOFANIKIWA
Mitandao ya kijamii kama X (zamani Twitter), Facebook, na YouTube imekua ikiripoti kwamba mara nyingi Wanawake wana uwezo wa kuongoza kwa ufanisi sawa na wanaume.
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Baada ya kuapishwa kuwa Rais mwaka 2021 alisimamia ujenzi wa miundombinu mikubwa, diplomasia ya kimataifa, na kuleta maridhiano ya kisiasa nchini.
utafiti uliochapishwa mwaka 2023 kwenye jarida la Information, Communication and Society, umeonyesha kuwa mawasiliano yake kupitia mitandao ya kijamii yalijenga taswira nzuri ya uongozi wa mwanamke.
Bi Ellen Johnson Sirleaf Rais wa zamani wa Liberia na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, aliyefanikiwa kuleta amani na kujenga upya nchi yake iliyotoka kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Jacinda Ardern Waziri Mkuu wa zamani wa New Zealand, aliyetambulika kwa uongozi wake thabiti na wenye huruma wakati wa majanga ya kitaifa kama shambulio la msikitini na janga la Uviko-19.
TAKWIMU
Zanzibar wapo Madiwani wanawake 27 kati ya
Madiwani wote 110 ambapo kwa mkoa wa Kaskazini Pemba Pekee wapo madiwani 34.
MIKATABA
Katiba
ya Zanzibar ya 1984, Kifungu cha 21 kifunu kidogo cha 3 kinaeleza kwamba, kila mzanzibari
anayohaki ya kushika nafasi yoyote ya kazi na shughuli yoyote iliyoko chini ya
mamlaka ya Zanzibar.
Mkataba
wa Umoja wa Mataifa wa kutokomeza ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW) wa mwaka
1979, hususan Kifungu cha 7, kinachotaka wanawake washiriki kikamilifu katika
maisha ya kisiasa na ya umma.
Azimio la Beijing (Beijing Declaration and Platform for Action) la mwaka 1995, linalosisitiza kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za maamuzi.
Itifaki ya Maputo ya mwaka 2003, Kifungu cha 9, kinachohimiza ushiriki sawa wa wanawake katika mchakato wa kisiasa na maamuzi.
MWISHO
.jpg)
Comments
Post a Comment