KILIMO MSITU TARAJIO LA KUJIKOMBOA NA UMSKINI
NA FATMA HAMAD, PEMBA MKURUGENZI WA Jumuia ya uhifadhi Mazingira Pemba CFP Mbarouk Mussa Omar amezitaka kamati zinazosimamia masuala ya uhifadhi wa mazingira kuhakikisha wanaendeleza shughuli hizo ikiwemo kilimo msitu, ili kuona wanajipatia kipato. Mkurugenzi huyo ameyasema hayo wakati akizungumza na wanakamati hao ambao ni kutoka shehia za Chwale, Kambini kichokochwe, Kiuyu na Mchangamdogo katika mafunzo ya siku mbili ya kuweka mikakati madhubuti ya kuendeleza shughuli za uhifadhi mazingira,yaliofanyika Ofisi za CFP huko Minyenyeni mkoa wa Kaskazini Pemba. Alisema kilimo ndio tegemeo kubwa la Taifa, hivyo ni vyema wanakamati hao kuendelea kulima kilimo msitu, waweze kuzalisha mazao ambayo yatawasaidia kupata chakula pamoja na pesa ambazo zitaendesha maisha yao. ‘’Ndugu zangu shughuli hizi za kulima kilimo msitu msifanye kwa sababu tu ya mradi, bali ifanyeni kama ni kazi yenu ya kila siku, kwani mukifanya hivyo mtapata mazao mtakula nyumbani na...