WANDISHI JISOGEZENI KWA WATAFITI, MUIBUE KERO ZA JAMII

 

NA FATMA HAMAD, PEMBA

 Wandishi wa Habari wametakiwa  kuzitumia Tafiti wakati wanapoandika habari zao, ili kuibua changamoto zinazoikabili jamii na kupatikana kwa ufumbuzi wa  jambo husika.

 Ushauri huo umetolewa na commissiona wa ufuatiliaji na tathmini kutoka Tume ya Mipango Zanzibar zuhura Mohd Abdallah kwa niaba ya katibu mtendaji wakati  akifungua mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari, yaliyofanyika  ZRA Gombani Chakechake mkoa wa Kusini pemba.

Alisema wandishi wa Habari wanasauti kubwa katika jamii, hivyo, endapo watazitumia tafiti mbalimbali zinazofanywa wakati wakiandika habari zao, wataibua matatizo yanayowakumba wanajamii  na kufanyiwa kazi kusaidia kupatikana kwa maendeleo Nchini

  Aidha alisema Tume ya mipango  Zanziba imeona ipo haja kutoa mafunzo hayo ya utafiti kwa Wandishi wa habari kwani kutawaongezea uwelewa wa kufahamu mbinu za

uandishi wa habari za uchambuzi, zilizofanyiwa utafiti kwa manufaa ya jamii na taifa

 ‘’Wandishi wa Habari ni watu muhimu katika jamii, hivyo endapo mtazitumia na kuzichambua tafiti jamii ikazielewa na kuzifazifanyia kazi  watatatua changamoto zinazo wakabili kwa asilimia kubwa,’’alisema.

Mapema  Mhadhir kutoka chuuo kikuu cha Dar- es - salaam  Egbert Mkoko na alisema kuwa habari za utafiti zina nafasi kubwa katika kuibua ukweli na kufichua kero zilizojificha zilizojificha katika jamii.

 ‘’Wandishi wa Habari wasiogope kuzitumia tafiti kwani wataisaidia jamii kuondokana na shida ambao zimewakabili vijijini mwao,’’alishauri.

 Kwa upande wake Mtaalamu wa masuala ya kihabari  kutoka Zanziba Ali Sultan alisema bado Wandishi wa habari hawajajikita zaidi kuandika habari za utafiti, hivyo ni budi kwa mazingira ya sasa kuacha kuandika habari kimazoea, wazitumie tafiti ili wawe mkombozi katika jamii.

 Nao baadhi ya waandishi walioshiriki katika mafunzo hayo walisema ni jambo lafaraja kuona tume hiyo imeona umuhimu wakutoa mafunzo hayo ambayo

 Yatawawezesha  waandishi wa habari kufanya shughuli zao kwa ufanisi Zaidi.

MWISHO

 

Comments

Popular posts from this blog

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

UROHO WA MALI KWA WANAUME UNAVYONYIMA WANAWAKE ARDHI

‘’KATIBU MKUU ELIMU ‘’TOENI ELIMU YA MALEZI BORA’’