WANANCHI WALIOCHUKULIWA ARDHI ZAO WAOMBA KULIPWA FIDIA ZAO

 WANANCHI KISIWANI Pemba ambao walichukuliwa Ardhi zao kwa ajili ya Ujenzi wa Miradi ya Maendeleo na Uwekezaji waliokua hawajalipwa fidia zao wameiomba Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi kuwasikiliza kilio chao na kuwafuatilia ili wapate haki zao serikalini.

 Akizungumza katika kikao cha Uwasilishaji wa Ripoti ya Uandaaji wa Sheria ya Sekta Miliki Zanzibar kilichofanyika Gombani Chakechake Pemba, Suleiman Mansur mwananchi wa Chakechake alisema tokea alipochukuliwa ardhi yake kwa ujenzi wa Skuli ya Uwandani bado hajalipwa fidia yake.

 Alisema kila siku amekua akihangaika kwa ajili ya kutafuta haki yake, lakini ameshindwa, hivyo  aliomba Wiazara ya Ardhi kuwafuatilia kero lao na kuwaonesha njia ya kupita, ili kuona wanapata haki zao,

 ‘’Kila siku nahangaishwa mara peleka barua kwa mkuu wa Wilaya mara Mkoa wala sjaona lolote, tunawaomba wenzetu wa wizara ardhi mtusaidie tupate fidia zetu,alisema.

‘’’alisema,

 Kwa upande wake wakili wa kujitegemea  kutoka Chake chake Zahran Mohammed Yussuf ambae alishiriki kikao hicho, alisema ni vyema kuwepo na Mamlaka moja tu ambayo inatoa hatimiliki kwa wananchi, jambo litalosaidia kupunguza migogoro ya Ardhi katika Jamii.

 ‘’Utakuta kuna BPR, Wokfu, Wizara ya Ardhi, zote zinatoa umiliki ardhi, hivyo kuepo kwa mlolongo wa Taasisi kunachangia migogoro, ni vyema serikali kuweka mamlaka moja tu,’’alisema.

 Mapema Muezeshaji wa kikao hicho Ali Ali Hassan alisema kwa mujibu wa kifungu cha 17 (C) cha Katiba ya Zanzibar yam waka 1984  kinasema mwananchi anatakiwa alipwe fidia  yake kabla ya ujenzi kuanza na inayolingana na mali yenyewe.

 Hivyo aliwataka wananchi hao ambao wanadai fidia zao kuenda Mahkamani na kudai haki zao.

 Afisa Mdhamini wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Bakar Ali Bakar, alisema kuepo kwa Sheria ya Sekta Miliki Zanzibar

kutasaidia kuondokana na migogoro ya ardhi Nchini.

 MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

UROHO WA MALI KWA WANAUME UNAVYONYIMA WANAWAKE ARDHI

‘’KATIBU MKUU ELIMU ‘’TOENI ELIMU YA MALEZI BORA’’