Posts

Showing posts from August, 2026

ZRA yafanya mabadiliko Sheria za Kodi

Image
  NA ZUHURA JUMA, PEMBA SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imekuwa ikifanya mabadiliko ya Sheria za kodi, ili kuleta unafuu kwa walipakodi sambamba na kupatikana kodi vizuri. Akizungumzia Sheria zilizofanyiwa maboresho, Ofisa Kitengo cha Habari, Uhusiano na Huduma kwa Walipa Kodi, kutoka Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA), Makame Khamis Mohamed alisema, kabla ya kurekebishwa Sheria, Serikali hufanya utafiti kwanza ili zisimuathiri mlipakodi wala Serikali. Alisema kuwa, hatua hiyo ya kuzifanyia maboresho Sheria za kodi ni katika kuwajali wananchi wake, kwani kuna baadhi ya vitu vimeondolewa ushuru na vyengine vimepunguzwa kwa asilimia 25, jambo ambalo litasaidia sana katika kuboresha utekelezaji wao wa majukumu, pamoja na kuleta unafuu kwa walipakodi. “Mabadiliko haya yamekuja kuleta unafuu kwa walipakodi na wananchi kwa ujumla, hivyo kama waandishi wa habari tunapaswa kuuhabarisha umma, ili waelewe maboresho haya na kuyafanyia kazi,” alisema Makame. Alieleza kuwa, lengo la kufanyia mabor...

NAJIVUNIA KUONA WANANCHI WA MJINI KIUYU WAKIKANYAGA BARABARA YA LAMI

Image
                                          NA FATMA HAMAD, PEMBA                                                                                                                             ‘’Ama kweli mwenye kutafuta haachi kupata’’ Msemo huo umesadilifu kwa Nassra  Salim Mohamed Diwani mstaaf wa wadi ya Kiuyu Minungwini wilaya ya Wete mkoa wa Kaskazini Pemba. MAISHA YA NASRA Baada ya kuzaliwa  1969, Nasra alianza kuisaka haki ya elimu ya msingi mwaka 1976 katika skuli ya msingi Piki wilaya Wete. Akiwa darasani, Nasra hakuwa mtulivu na jinsia yake ya kike, wak...

ALIANZIA UWAZIRI WA WANAWAKE NA WATOTO WA SERIKALI YA WANAFUNZI NA SASA UKATIBU TAWALA

Image
              NA FATMA HAMAD,PEMBA   ‘’Sitoisahau siku nilioteuliwa nafasi ya  Ukatibu Tawala’’. Hayo ni maneno ya Bi Mkufu Faki Ali (51) ambae ni Katibu tawala wilaya ya Wete mkoa wa Kaskazini Pemba Kwa hofu aliokua  nayo mwanzoni nafasi hiyo hakuifurahia, kwani alihisi ni nafasi kubwa kwake. ‘’Watu wakipata uteuzi huwa wanafurahia, ila sikufichi  mimi sikuile ya  mwanzo nilishindwa hata kula nilikua nikilia,’’anasema. Aliteuliwa Octoba 2017 kipindi hicho alikua mfanya kazi wa Tume ya Uchaguzi  wilaya Wete Kaskazini Pemba. Nafasi hiyo ilimuia vigumu, kwani ilikua bado ni mdogo, akiangalia anaowaongoza anaona wengine ni watu wanaomzidi na anaowaheshimu ‘’Nilipokua Chuoni nilikuwa Waziri wa Wanawake na watoto na niliiweza, hivyo nikajipa moyo na hiyi nitaiweza,’’alifahamisha. Mwana mama huyo aliezaliwa mwaka 1973, kijiji cha Utaani, kwasa anaishi Kizimbani wilaya ya Wete, Safari yake ya utumishi, ilianzia katika taaluma ya ...