ALIANZIA UWAZIRI WA WANAWAKE NA WATOTOU WA SERIKALI YA WANAFUNZI NA SASA UKATIBU TAWALA
NA FATMA HAMAD,PEMBA
‘’Sitoisahau siku nilioteuliwa nafasi ya Ukatibu Tawala’’.
Hayo
ni maneno ya Bi Mkufu Faki Ali (51) ambae ni Katibu tawala wilaya ya Wete mkoa
wa Kaskazini Pemba
Kwa
hofu aliokua nayo mwanzoni nafasi hiyo
hakuifurahia, kwani alihisi ni nafasi kubwa kwake.
‘’Watu
wakipata uteuzi huwa wanafurahia, ila sikufichi
mimi sikuile ya mwanzo
nilishindwa hata kula nilikua nikilia,’’anasema.
Aliteuliwa
Octoba 2017 kipindi hicho alikua mfanya kazi wa Tume ya Uchaguzi wilaya Wete Kaskazini Pemba.
Nafasi
hiyo ilimuia vigumu, kwani ilikua bado ni mdogo, akiangalia anaowaongoza anaona
wengine ni watu wanaomzidi na anaowaheshimu
‘’Nilipokua
Chuoni nilikuwa Waziri wa Wanawake na watoto na niliiweza, hivyo nikajipa moyo
na hiyi nitaiweza,’’alifahamisha.
Mwana mama huyo aliezaliwa
mwaka 1973, kijiji cha Utaani, kwasa anaishi Kizimbani wilaya ya Wete, Safari
yake ya utumishi, ilianzia katika taaluma ya uwalimu.
SAFARI
YA KUELEKEA KWENYE UONGOZI
Mwaka
1980 alianza masomo katika skuli ya
Msingi Kizimbani, na baada ya miaka
saba, aliingia Utaani Sekondari kuendeleza na elimu yake.
Mnamo mwaka 1990 alimaliza masomo yake ya darasa la 11 ingawa hakubahatika kuingia darasa la 12.
Kufeli kwake hakukumfanya apoteze tumaini, alijipanga upya, alijiunga na Chuo cha Ufundi Dodeani Wingwi ili atimize ndoto zake.
‘’Hapo Ufundi nilianza darasa la tisa hadi la 12 nikafanya mtihani nikafaulu nikabahatika kuingia Fom iv skuli ya Fidel Castro iliyopoChakechake,’’ anafahamisha.
Aliendelea kukata viatu akiisaka elimu kwa hali na mali, mwaka 1996 alijiunga rasmi na Chuo cha uwalimu Nkurumah, katika ngazi ya cheti.
Alipoingia Chuoni hapo tu, alianza kujifunza majukumu ya Uongozi, kwani, alikua Waziri wa wanawake na watoto kwa kipindi chote alichokuwepo hapo.
‘’Nilikua sipendi kukaa nyumanyuma na ndio maana nikachaguliwa nafasi hiyo na niliitumikia kama inyotakikana,’’anasema.
Mnamo mwaka 1998 alianza kuvuna matunda, aliajiriwa na kufundisha katika skuli ya Jadida iliopo Wete Pemba.
‘’Nilipoanza kuonja matunda hayo utamu ulinichachukia, baada ya miaka nane, nilijiunga tena na Chuo cha Uwalimu cha Nkuruma katika ngazi ya Diploma na nikamaliza mwaka 2007,’’anasema.
Hakutosheka na hapo kwavile alikua na ndoto za kufika mbali, mwaka 2008 alijiunga na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania katika ngazi ya Shahada ya kwanza.
Ilipofika 2015 alijihisi hajafika sehemu anayoitaka, alijichukulia shahada ya pili ya Huduma za Jamii (MASTER OF SOCIAL WORK) katika Chuo kikuu Huria na kumaliza mwaka 2020.
Baada ya kumaliza masomo yake, akiwa anaendelea na majukumu yake ua Uwalimu, alipata uhamisho kutoka skuli ya Jadida, na kupelekwa Limbani Wete.
Hapo ndipo alipoanza kuonesha uwezo wake wa kufanya kazi kwa bidii, kwani ilikua ndo mwalimu mdogo kuliko wote.
‘’Iilikua wananituma mara tupikie chai, tusafishie, tukoshee vyombo, nilikua ninawatumikia kwa furaha na kwa tabasamu,’’anasimulia.
Yote hayo hakua akichoka, alifanya kazi yake kwa imani na hilo lilimjengea heshima na kufikia mwaka 2007 alipelekwa Tume ya Uchaguzi na kuwa Msaidizi Afisa Uandikishaji wa wilaya,’’anaeleza.
‘’Kumbe vile nilivyonikifanyiwa ilikua mtihani, nashukuru niliufaulu, na mwaka 2017 serikli iliniamini, ikaniteua nafasi ya Ukatibu Tawala wilaya ya Wete.
Mwanzoni baada ya kupata nafasi hiyo aliogopa, kwani wilaya ya Wete, ilikua na watu ambao walikua na misimamo na mihemko ya kisiasa.
‘’Ingawa nilikua na hofu, ila nilijenga uthubutu, nimeitumikia vyema nafasi hii wananchi wananikubali wananiamini,’anasema.
Hatimae ulemsemo unaosema ‘nyotanjema huonekana alfajiri; kwa Bi Mkufu umesadifu, kwani nafasi hile alioanza kuitumikia akiwa chuoni, imekua ufunguzi wa yeye kuendelea kuwa kiongozi.
Tokea apate nafasi hiyo ameshakaa na wakuu wa wilaya zaidi ya watatu, amekua akifanyakazi zake kwa uangalifu, hajawahi kukwaruzana nao.
ANAYOJIVUNIA
Moja
analojivunia katika uongozi wake ni kuimarisha uhusiano wa kijamii, kuishi kwa
upendo na mshikamano, na kushiriki kwa pamoja katika shughuli za maendeleo.
‘’Mji wa Wete ulikua ni mithili ya moto wa kifuu, ila nimeutuliza, wananchi wanikubali na tunaishi kwa amani, kwa upendo,’’anasimulia.
Mbali na hilo, amekua akiwasadia mitaji wananchi wanyonge, wafanye shughuli za kiuchumi wajipatie kipato waendeshe familia zao.
‘’Akinijia mwananchi nimsaidie sioni tabu, natoa pesa zangu, nampatia mtaji afanye biashara
ajipatie
kipato aendeshe maisha yake,’anaeleza.
Sambamba na nafasi hiyo alishawahi kuteuliwa kuwa Mshauri wa Kamati za shehia, Mlezi wa Madrasa mbalimbali za Wete.
CHANGAMOTO KATIKA KAZI
Maranyingi vikwazo
vinavyomkwaza katika uongozi wake ni nidharau nakuitwa maneno mabaya na baadhi
ya watu wasiopenda maendeleo ya wanawake.
‘‘Wapo
baadhi ya watu hunidharau na hunipa maneno yanye kunikatisha tamaa,’’anasema.
WATU WANAOMFAHAMU
Salma Saleh Hamad Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya
Wete, uongozi Katibu Tawala wao Bi Mkufu umewakomboa kwani wanapata fursa
mbalimbali ikiwemo likizo.
‘’Tulikua stahiki zetu tunazikosa, likizo, na ‘Overtime’ tulikua hatupati hapo kabla ya uongozi wake Bi Mkufu,’’anasema.
Mohamed Hamad Ali mlinzi wa Ofisi ya mkuu wa Wilaya, anasema uongozi wa Bi Mkufu ni wa mfano, kwani anawajali na amekua na tabia ya kuwaweka vikao akisikiliza kero zao.
‘’Kama kuna nafasi ya Mkuu wa Mkoa, basi tunaomba apewe, mama huyu anajitahidi, ni muadilifu
anaongoza kwa hekima,’’anafahamisha.
MASHEHA
Omar Khamis Othman Sheha wa Kiungoni, anasema Mkufu ni kiongozi anaefanya kazi kwa bidi, anafuatia wafanyakazi wake, simbaguzi, anajali utu.
‘’Mamayetu huyu ni mchapa kazi, hapendi kukaa tu Ofisini anafuatilia kazi zetu, anapenda umoja na wala hana ubaguzi na yoyote,’’anasema.
Ramia Said Rashid sheha wa Bopwe, anasema yeye Bi Mkufu anamuona anafaa kwa kiongozi, kwani anajiamini, na anapambana kila hali, katika kutatua shida za wananchi.
Mkuu wa wilaya ya Wete Abdalla Rashid Ali anasema Mkufu ni kiongozi imara, mchapa kazi na anajali kazi yake pamoja na watendaji.
‘’Huyu mwanamama yuko vizuri,ni mfano tosha kwa
viongozi wanawake, nafurahi hata mimi nilipokwenda alinipokea vizur,’’anasema.
Hakujifanya kama ni
kiongozi wa serikali tu, bali anabeba nafasi ya umama katika jamii yake, akisikia
kuna jambo Fulani analifuatilia hadi anahakikisha amelipatia ufumbuzi.
Namsifia hasa kwani
amechukua nyayo za kiongozi wetu mamayetu Samia Suluhu Hassan, amekua habagui,
hachagui anajali maendeleo kwa wote.
WANAHARAKATI
Afisa program kutoka Chama cha Wandishi wa Habari wanawake Tanzani ( TAMWA ZANZ) Khairat Ali anasema, uwepo wa viongozi wanawake ni hatua muhimu katika nchi.
‘’Uwakilishi wa wanawake katika maamuzi unasaidia kubadilisha sera, ingawa bado kunachangamoto za kimfumo na mitazamo tofauti kuhusu kasi ya mabadiliko hayo,’’anasema.
MIKATABA
Ripoti na Mitazamo ya Mitandao ya kijami inasema maranyingi wanawake huleta mabadiliko wanapopewa nafasi, kwani hutumia busara, ushawishi, kutatua migogoro na kuleta utulivu katika jamii zao.
Ilani ya Uchaguzi na
serikali za mitaa ya mwaka 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020
inalenga serikali kuu iliyoko madarakani na ile itakayoshika madaraka na
taasisi zake, ina wajibu wa kuhakikisha kuwa uwanja wa ushindani wa kisiasa ni
huru na wa salama kwa makundi yote hususani wanawake.
Mkataba wa kimataifa wa haki za kiraia na haki
za kisiasa ya mwaka 1976 kifungu cha 25, kinaeleza kila raia ana haki ya kupiga kura na
kuchaguliwa katika uchaguzi wa kweli, wa haki na wa mara kwa mara, uliofanywa
kwa kura ya siri.
Hata Katiba ya Zanzibar
ya 1984, ambayo ndo sharia mama, kupitia kifungu chake cha 21(1) nacho
kinatambua haki ya kila raia kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi bila
ubaguzi.
Dira ya Maendeleo ya 2050
inasema Usalama na usawa wa kijinsia ni nguzo kuu katika mabadiliko ya kijamii
na utekelezaji wa sera za nchi.
Kisiwa cha Pemba
inazowilaya nne, ikiwa Makatibu Tawala
wilaya ni sawa kati ya wanaume na wanake.
MWISHO
Comments
Post a Comment