
Waandishi wa habari
Pemba wametakia kuibua na kuandika habari zinazochangia kufanyika kwa vitendo vya
udhalilishaji katika maeneo yasio maarufu (yasio tambulika).
Agizo hilo limetolewa na
Mratibu wa Mradi wa Tunaweza pamoja kutoka Tamwa Zanzibar Asya Hakim
Makame katika mafunzo ya siku mbili kwa
waandishi wa habari wa vyombo
mbalimbali,yaliyofanyika Ofisi za TAMWA Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
Alisema yapomaeneo kadhaa ambayo wanawake na watoto wamekua
wakidhalilishwa kama vile kwenye usafiri wa Umma, Bandarini, Masokoni na hata
katika mitandao ya kijamii, na hata kwenye viwanja vya Skukuu za Iddi.
Alisema licha ya udhalilishaji unaofanywa katika sehemu hizo,
lakini bado wandishi wa habari hawaripoti, hivyo ipo haja kwa sasa kutupa jicho
lao na kuibua kesi hizo, ili kuona usalama unatawala ndani ya maeneo hayo
ambayo sio rasmi.
‘’Wandishi wa habari msiishie tu kuandika udhalilishaji
unaofanywa Madrsa, Mitaani,amma
Maskulini, bali jikiteni masokono,
bandarini, kwenye daladala na hata katika mitandao ya kijamii ili nako huko
kubaki salama,’’alisema.
Kwa upande wake Mkufunzi wa mafunzo hayo toa Haji Nassor Moh’d alisema miongoni mwa vitendo
hivyo vya udhalilishaji ambavyo vimekua vikifanyika ni pamoja na usafirishaji
haramu wa binaadamu.
Aidha alisema bado takwimu zinaonesha kuongezeka kwa matukio ya udhalilishaji kwa wanawake na
watoto visiwani Zanziba.
Alisema Takwimu kutoka Ofisi ya Mtakuimu mkuu wa serikali ya
Zanziba Machi 2026 kuliripotiwa matukio 103 ya ukatili na udhalilishaji, ambapo
watoto ilikua ni 84 sawa na asilimia 81.6 wanawake wakiwa ni 17 sawa na
asilimia 16.5.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo walisema mafunzo yatawasaidia katika majukumu yao kwani
watatumia kalamu zao kuelimisha jamii juu ya vitendo vya udhalilishaji
vinavyoendelea kutokea kwenye maeneo hayo ambayo sio rasmi.
Mafunzo hayo kwa waandishi wa habari ni sehemu ya utekelezaji wa
mradi wa "Tunaweza Pamoja" unaotekelezwa ma UN Women kwa kushirikiana
na TAMWA Zanzibar kwa ufadhili wa Serikali ya Norway chini ya mpango wa Umoja
wa Mataifa unaolenga kujenga jamii salama dhidi ya vitendo vya udhalilishaji
kwa wanawake na wasichana.
Mradi huo wa Tunaweza pamoja unatekelezwa katika Mikoa ya
Kaskazini mwa Pemba na Unguja, ambao unalengo la kuondosha vitendo vya
udhalilishaji kwa wanawake na wasichana.
MWISHO.
Comments
Post a Comment