NA FATMA HAMAD PEMBA.
Wandishi wa
habari wamehimizwa kuendelea
kutumia nafasi zao kuihamasisha jamii kushiriki zoezi la Sensa ya watu na makazi ambalo linatarajiwa kuanza
hivi karibuni .
Wito huo
umetolewa na Kamisaa wa sensa
Zanzibar Balozi Mohd
Haji Hamza wakati akizungumza na wandishi wa habari
katika mkutano ulioandaliwa na Ofisi ya Mtakuimu mkuu wa Serikali Zanzibar
huko Jamhuri Holli Wete Pemba.
Balozi Hamza
amesema vyombo vya habari vinamchango mkubwa katika kuendesha shughuli mbali
mbali za Nchi, hivyo ni wakati wenu sasa kuwaelimisha Wananchi juu ya suala
zima la sasa ili waweze kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo.
‘’Wandishi
wa habari tumieni sauti zenu na kalamu zenu
kuwashajiisha Jamii juu ya kushiriki zoezi zima la sensza ya watu na makazi na kuhakikisha wanatoa
tarifa sahihi’’ amesema kamisaa wa sense.
Amesema Sensa ya watu na makazi hufanyika kila baada
ya miaka kumi [10] ambapo lengo kuu
la kuepo
kwa zoezi hilo ni kujua idadi ya
watu waliomo Nchini.
Aidha
amefahamisha kuwa usiku ule wa kuamkia siku
ya zoezi hilo watu watakaolala katika kaya moja watahesabiwa wote
bila ya kujali uraia wa mtu, awe mtanzania ama asiekua mtanzania.
Nae afisa
mdhamini wizara ya habari utamaduni
Vijana na Michezo Mfamau Lali Mfamau
amemuahidi kamisaa wa sensa
kupitia wizara yake kwamba wataungamokono kuanzia mwanzo hadi mwisho
kuhakikisha zoezi hilo limemalizika kwa amani kama ilivyo
tarajiwa.
Sensa ya
mwaka huu ni sense ya Sita tokea kupatikana kwa
uhuru wa Nchi hii.
Comments
Post a Comment