KIRARE BADO AISOTEA RUMANDE

 


FATMA HAMAD PEMBA.

Mahakama ya mkoa B iliopo Kusini Pemba imeghairisha kesi

ya kuingilia kinyume na maumbile inayomkabili kijana

Khamis Abdala Khamis marufu kirare mwenye umri wa

[20] mkaazi wa Kangani wilaya ya Mkoani baada ya

mtuhumiwa huyo kukataa kusomewa shitaka lake .

Kijana huyo wakati akiwa ametulia kizimbani na kusubiri

asomewe shitaka lake aliambia mahakama hiyo kuwa hali

yake sio mzuri anaomba kesi ighairishwe na ipangiwe siku

nyengine.

‘’Mheshimiwa hakimu leo naumwa siwezi kukakaa hivyo

naiomba mahakama yako ighairishe shauri hilo kwa leo’’

alieleza mtuhumiwa kirare.

Hakimu wa mahakama hiyo Muumin Ali Juma  amesema hii ni mara ya pili unasema unaumwa  daktari anakuja na kurudi ila ujue baadae fursa hii hutoipata tena nitakua sikusikilizi tena , na mahakama itatoa oda ya kumruhusu daktari afanye shughuli zake mpaka utakapo kuwa tayari  ndio tutamleta na wewe  utarudi rumande hadi tarehe 9/ 8 2022kwa ajili ya kusikiliza mashahidi.

Mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo siku ya rehe 28/ 5/2022 ya

smbili za usiku huko kangani Sokoni wilaya ya Mkoani bila ya

halali na bila ya ridhaa ya walezi wake alimtorosha Mtoto wa

miaka 10 kutoka sokoni alipokua amekaa na kumpeleka

kwenye banda ambalo anaishi, na siku hiyo hiyo wakati wa 2;

7 usiku ulimuingilia kinyume na maumbile ambapo kufanya

hivyo ni kosa kinyume na kifungu cha 115 cha sharia namba 6 / 2018 sheria  ya Zanzibar.


 

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.