mbunge wa wawi aekeza kwenye sekta ya michezo
Uwanja wa
mpira wa miguu wa mtega uliopo Wilaya ya Chake Mkoa wa kusini Pemba umeanza kufanyiwa matengenezo
ili kuona unachezeka na unatumika muda wote.
Akizungumza
na wandishi wa habari mbele ya
ukarabati huo Mbunge wa jimbo la Wawi Khamis Kassim Ali kupitia chama cha Mapinduzi Amesema
takribani miaka 45 uwanja
huo umeonekana kuchakaa
hivyo ameamua kufanyia
ukarabati ili uwe uwanja ambao unaendana
kimichezo.
‘’Nimeamua
kutengeneza uwanja huu ili kuwaondoshea changamoto vijana ambao wameamua kuwekeza katika
michezo’’ alieleza mbunge.
Hivyo Ametaka
wanamichezo hao kuutunza na kuulinda
uwanja huo ambao utaleta manufaa
kwao na kwa kizazi chao.
Aidha mbunge huyo amesema suala la mpira kwa sasa ni ajira, hivyo ni wakati vijana kuchangamkia fursa hiyo kwani kutawawezesha kujipatia kipato.
kwa upande wake katibu wa timu ya Wawi star Juma Muhammed Tamimu amesema mategemeo yao ni kuona kwamba uwanja wao umekuwa uwanja wa kisasa kama ilivyo viwanja vyengine.
Hichi ni
kiwanja cha nne kufanyiwa ukarabati na
mbunge huyo ikiwa ni pamoja na kiwanja cha ndugu kitu, Gombani ya kale na Nyungu nyungu .
Comments
Post a Comment