KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME
NA FATMA HAMAD- PEMBA
WANANCHI WA KIJIJI cha Gombeume
Shehia ya Mchangamdogo Wilaya ya
Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, wamelalamikia juu ya ukosefu wa huduma ya
Maji safi na
salama
kijijini hapo.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi huko kijijini kwao Gombeume mwananchi Bishamba
Suleiman Ali na Fatma Said Haji wamesema
huu ni zaidi ya mwaka wa tatu hawapati huduma ya maji katika kijiji chao.
Walisema
wamechoka na kadhiya hiyo ambayo inawafanya waende mabondeni kufuata huduma ya maji, kwa ajili
ya matumizi ya majumbani
mwao.
‘’Kwakweli
tuna shida kubwa wananchi wa gombeume, tunakwenda mabondeni kwenye visima vya
zamani kuchota maji, tunaumia na
tumechoshwa na shida hiyo,’’walisema.
Walisema
wanahofu ya kujakupata maradhi ya
mripuko, kutokana na kukosa maji ya
kutosha ya kufanyia usafi kwenye vyovyao ambavyo wanatumia majumbani mwao pamoja na misikitini.
‘’Tunashindwa
kupata hata maji ya kufanyia usafi majumbani mwetu, mungu tu mwenyewe atulinde
na maradhi,’’walisema.
Kwa upande
wake Bi Mtumwa Makame alisema tatizo la
maji limekua kubwa na limekua kero, kwani hata wanapopatwa na msiba wanakuwa na
hofu ya kupata maji na kuweza kumsitiri mwenzao.
‘’Ni juzi tu
alikufa jiraji nyumba hile pale, ili
tubidi tuende mabondeni kubeba maji ya kuja kumsitiri mwenzetu, jee hiyo ni
hali kweli,’’alieleza.
Nae
mwananchi Bakar Khamis Bakar alisema
kuwa Tatizo limekua kubwa, jambo linalopelekea wanawake wa kijiji
hicho kukosa kufanya shughuli za uzalishaji, kwani hupoteza muda mwingi wakiwa
visimani, kwa ajili ya kutafuta maji.
‘’Tokea
kutakapokucha wanawake wa kijiji
hichi wao ni kuhangaika mabondeni tu na
ndoo za maji, hawapati kufanya shughulinyengine yeyote
ya kujingizia kipato, tunahitaji kuwangaliwa na kufanyiwa
msaada tunaumia,’’alisema.
Afisa wa Mamlaka ya Maji Safi na Salama Zanzibar (ZAWA ) kisiwani Pemba Suleiman Anass Masoud alikiri kuepo kwa tatizo hilo kijijini hapo.
Alisema kwa sasa tayari wameshapeleka mashine katika
kisima kilichopo kijiji cha kibomani, ambacho kitasambaza maji maeneo yote ya
mchangamdogo, na Gombeume.
Hivyo
amewataka wananchi kuwa na uvumilivu kwani mafundi wako kwenye matengenezo, ya
miundombinu, ili kuona wananchi hao
wanaondokana na kadhya hiyo.
Aidha Afisa huyo alisema kwa maeneyo mengi
ambayo yamekua yakikosa maji kutokana na ujenzi wa barabara, sio tatizo la Mamlaka ya Maji, kwani wao
hutoa maelekezo ili kuona wananchi
hawathiriki kwa ajili ya ujenzi huo.
‘’Kwa maeneo
yote ambayo wananchi hawapati maji kwa kutokana na ujenzi wa barabara, sisi sio
jukumu letu zawa, sisi tunawaeleza vya kutosha watakapojenga wasikate
miundombinu ya maji, kwani itakua ni usumbufu kwa wanachi,’’alieleza.

Comments
Post a Comment