WANDISHI WA HABARI WAPEWA RUNGU PEMBA

 

'IMG-20220708-WA0003.jpg' failed to upload. TransportError: There was an error during the transport or processing of this request. Error code = 103, Path = /_/BloggerUi/data/batchexecute

Wandishi  wa  habari  wamehimizwa   kuendelea  kutumia nafasi   zao  kuihamasisha jamii  kushiriki zoezi la Sensa  ya watu na makazi ambalo linatarajiwa kuanza hivi karibuni .

Wito huo umetolewa na Kamisaa  wa  sensa  Zanzibar  Balozi  Mohd  Haji  Hamza  wakati akizungumza na wandishi wa habari katika  mkutano ulioandaliwa na  Ofisi ya Mtakuimu mkuu wa Serikali  Zanzibar  huko  Jamhuri Holli Wete  Pemba.

Balozi Hamza amesema vyombo vya habari vinamchango mkubwa katika kuendesha shughuli mbali mbali za Nchi, hivyo ni wakati wenu sasa kuwaelimisha Wananchi juu ya suala zima la sasa ili waweze kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo.

‘’Wandishi wa habari tumieni sauti zenu na kalamu zenu  kuwashajiisha Jamii juu ya kushiriki zoezi zima la sensza  ya watu na makazi na kuhakikisha wanatoa tarifa sahihi’’ amesema kamisaa wa sense.

Amesema  Sensa ya watu na makazi hufanyika kila baada ya miaka kumi [10] ambapo  lengo kuu la  kuepo  kwa zoezi hilo ni  kujua idadi ya watu  waliomo Nchini.

Aidha amefahamisha kuwa usiku ule wa kuamkia siku  ya zoezi  hilo  watu  watakaolala katika kaya moja watahesabiwa wote bila ya kujali uraia wa mtu, awe mtanzania ama asiekua mtanzania.

Nae afisa mdhamini wizara ya habari utamaduni  Vijana na Michezo Mfamau Lali Mfamau  amemuahidi kamisaa wa sensa  kupitia wizara yake kwamba wataungamokono kuanzia mwanzo hadi mwisho kuhakikisha  zoezi  hilo limemalizika kwa amani kama ilivyo tarajiwa.

Sensa ya mwaka huu ni sense ya Sita tokea kupatikana kwa  uhuru wa Nchi hii.

 

 

 

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.