DK, MWINYI ALA SKUKUU NA MAYATIMA ZANZIBAR.

 


NA KAIJE SALUM ZANZIBAR.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK Hussein Ali Mwinyi amesema serikali itaendelea kushirikiana na taasisi mbali mabli za maendeleo kwajili ya kustawisha hali za wananchi.

Dk mwinyi ameyasema hayo huko maoustung katika ghafla ya chakula  kilicho jumuisha makundi mbali mbali wakiwemo watototo Mayatima.

Amesema kufuatia kuandaliwa kwa chakula hicho kunaashiria kuwepo kwa misingi ya upendo,mshikamano ni njia ya kuwathamini  Mayatima kuwa kama wale ambao hawajaondokewa na wazazi wao.

Amesema misingi ya imani na hali ya utulivu uliyopo kumepelekea kuwepo kwa mapenzi ya dhati kwa wadau ambao wanaguswa na watoto mayatima.


Amesema waislamu wanawajibu katika kuwahudumia Mayatima hivyo kulingana na maelekezo ya dini kuna faida kubwa katika kuwalea mayatima.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mandalizi ya ghafla hiyo   Mama Zainab Kombo Shaibu ametoa shukurani kwa wale wote waliyo saidia kufanikisha shughuli hiyo.


Ghafla hiyo ya chakula cha paomoja kwa watoto hao mayatima imeandaliwa na jumuiya ya Nuru  Foundation kwajili ya kuwafariji hasa katika kipindi hichi cha skukuu ya idil hajj. 




 


Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.