Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

 
 
                                               NA FATMA HAMAD PEMBA.

Wazazi na walezi wenye watoto  wenye ulemavu wamekumbushwa  kuacha tabia ya  kuwanyanyapaa na kuwafungia ndani  watoto hao, kwani kufanya hivyo ni udhalilishaji kwao.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Tumbe Mashariki katika mkutano maalumu Mkuu wa Polisi Jamii mkoa wa Kaskazini Abdala Majid Haji amesema wapo baadhi ya watu wamekuwa na itikadi potofu ya kuwachukulia watoto wenye ulemavu kama ni watu wasio na faida na badalayake huishia kuwafungia majumbani.

‘’Baadhi yetu hapa tunao watoto wetu wenye ulemavu tumewafungia tu ndani, hawatoki njee eti tunahofia jamii itatucheka,alisema.

Alisema Watoto wenye ulemavu nawao ni binadamu kama wengine wanastahiki kupata haki na fursa mbali mbali kama vile Elimu, Afya,Ajira.

 Alieleza kuwa ni wakati kwa wazazi wanaoishi na watoto wenye ulemavu  kubadilika na kuhakikisha wanatoa matunzo  sawa na wenzao  wengine wasio na ulemavu.

Alifahamisha  udhalilishaji sio tu kwa kubakwa au kulawitiwa bali hata kitendo cha kuwafungia ndani ni udhalilishaji kwa watoto hao.

 

Kwa upande wake Hidaya Mjaka Ali kutoka Umoja wa Wanawake wenye ulemavu Pemba alisema wapo baadhi ya watu wanapo zaa mtoto mwenye ulemavu wanahisi kama ni mzigo tu katika familia.

 Hivyo alisema ipo haja kutolewa Elimu kwa Jamii juu ya kuwalea na kuwatunza watoto wenye ulemavu, kwani nawao wana uwezo wa kufanya shughuli mbali mbali za kijamii ambazo zitaweza kuwaletea maendeleo.

 

Nae Mratibu wa Jumuiya ya watu wenye ulemavu wa akili Pemba [ZAPDD] Khalfan Amour Moh’d alisema kila mmoja ni mlemavu mtarajiwa, hivyo kila mtu kwa nafasi yake, cheyo chake kuwalinda na kuwaheshimu wato wenye ulemavu.

Aidha aliendelea kusema sio busara kuwatumikisha watoto wenye ulemavu, hususan wenye ulemavu wa akili kinyume na taratibu.

 

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.