Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.

 

 
 NA FATMA HAMAD,PEMBA

Mrajisi wa Mahakama  Zanzibar Valentina Andrew Catema amesema hawatomvumilia Hakimu yoyote atakae kwenda kinyume na  Sheria na taratibu katika utekelezaji wa majukumu yake.

 Mrajis huyo ameyasema hayo wakati akizungumza na Watendaji wa Mahakama ya Mkoani na Kengeja katika ziara malumu huko Ofisi za Mahakama ya Wilaya iliyopo Mkoani mkoa wa Kusini Pemba.

Amesema wapo baadhi ya Mahakimu wamekuwa na tabia ya Ucheleweshaji wa uwendeshaji na utoaji wa hukumu, jambo ambalo linapelekea watu kukata tama na kushindwa kufuatilia kesi zao.

‘ Kama hukumu inatakiwa itolewe ndani ya siku sitini basi uhakikishe unaitoa ndani ya kipindi hicho kinachotakiwa, vyenginevyo mtawajibika,alisema.

Aidha alieleza kuwa endapo watafanya majukumu yao kwa uwadilifu na sheria zinavyoelekeza kutaepusha kutokea kwa malalamiko, na kupelekea Wananchi kupata haki zao bila ya usumbufu.

 

Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhan Abdala amewasisitiza watendaji hao kuhakikisha wanatunza kumbukumbu za kesi zao, ili watu wanapokuja mahakamani kuangangalia ubini wao waweze kuzipata.

‘’Kuna wagombea wamekuwa wakikiwa pingamizi wakidaiwa kwamba  walishashitakiwa na kutiwa hatiani, na wanapokuja mahakamani kuangalia kumbu kumbu za kesi zao tunakuwa hatunazo, hivyo tujitahidi ili tusiwakoseshe watu haki zao,alieleza.

Alisema kuwa kuwa lengo la ziara hiyo ni kuzitembelea mahakama na kusikiliza changamoto zao ili waweze kuzifanyia kazi.

 Akitaja changamoto zinazowakabili mahakamani hapo Hakimu dhamana wa Mahakama ya wilaya Mkoani Suleiman Said Suleiman ni kutokuwa na choo cha nje kwa ajili ya Washtakiwa na watu wanaokuja kupata huduma, na kupelekea kutumia choo kimoja na wafanya kazi.  


 


 

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.