WEZI WA KARAFUU WATAKIONA MKUU WA MKOA ASEMA
Serikali ya
mkoa wa Kaskazini Pemba kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama mkoani humo imesema hawatomvumilia mtu yoyote
atakaefanya vitendo vya uhujumu
wa zao la karafuu katika
msimu wa mwaka huu.
Hayo
yamesemwa na mkuu wa wilaya ya micheweni Mgeni Khatib Yahya kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Kaskazini pemba
Salama Mbarouk Khatibu mbele ya Masheha
pamoja na wakulima wa karafuu mkoa
huo huko jamuhuri Holl Wete Pemba.
Amesema wakati wa msimu wa karafuu wapo watu
wanafanya ubabaishaji ikiwemo ununuaji karafuu za vikombe pamoja na uzwaji wa karafuu chafu katika vituo vya ZSTC.
‘’Niwambie
wezee wenzangu haipendezi kuonekana kwamba karafuu inanunuliwa na mchanganyiko
wa uchafu tunaona aibu kama sisi viongozi, hivyo kwa msimu huu hatutokua tayari
kuliona hilo tutahakikisha tumewafichua wote watakaofanya hivyo’’ alieleza mkuu
wa mkoa.
Wakitoa
changamoto ambazo zimekua zikiwaumiza
wakulima hao ni kuzuka kwa wizi na ukatwaji wa mikarauu kwenye mashamba
yao.
‘’Mheshimiwa
mkuu wa mkowa kwa kweli tunakilio wizi wanatumaliza na hawa wanaonunuwa karafu
za vikombe ndio wanaosababisha huu wizi’’ walieleza kwa masikitiko wakulima hao.
Aidha kwa
upande mwengine waliwasisitiza watendaji
wa shirika la biashara la ZSTC kuwa
wadilifu wakati wa majukumu yao hususan kipindi cha msimu jambo ambalo
litaondosha malalamiko kwa wakulima hao.
Comments
Post a Comment