HAKIMU AKATAA OMBI LA MBAKAJI.
Mtuhumiwa wa
kesi ya ubakaji
Mosi Othman Mosi
mkazi wa Mchakwe Muambe
ameiomba Mahakama kumfutia
shitaka lake kwa vile
shahidi ambae ndio muathirika
mwenyewe kushindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi.
‘’tarehe
iliyopita shahidi huyo hakuja, na leo hakuja
basi muheshimiwa hakimu bora kesi ifutwe ili nirudi zangu kijijini
niendelee na maisha yangu’’ alieleza mtuhumiwa mosi.
Hakimu wa
mahakama maalumu inayoshuhulikia kesi za ushalilishaji Mkoa wa kusini Pemba
Mumin Ali Juma alikataa ombi la mtuhumiwa huyo na kumuambia kuwa kesi hiyo
hawezi kuifuta, kwani kuna muda malumu uliowekwa kisheria kama mashahidi
hawakuja ifutwe ila hiyo haijafikia muda wa kufutwa.
‘’Si
kiubaliani na ombi hilo na kama shahidi huyo hakupatikana basi naomba aitwe
shahidi mwengine ili tuweze kusikiliza kesi’’ alisema hakimu Muumin.
Mtuhumiwa
Mosi Othman Mosi utaendelea kukaa rumande na utarudi tena mahakamani hapa tarehe 26/7/2022 kwa ajili ya kusikiliza
kesi.
Imedaiwa
mahakiamani hapo mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo siku na tarehe isiyofahamika
katika mwezi wa julai maka 2018 majira ya kumi usiku huko mchakwe Muambe wilaya
ya mkoani mkoa wa Kusini Pemba ulimbaka msichana wa miaka 15 ambapo kufanya
hivyo ni kosa kinyume na kifungu cha
108(1),(2)(e) na 109(1) sheria ya adhabu, Sheria namba 6 ya mwaka 2018, Sheria
ya Zanzibar.
Comments
Post a Comment