VIONGOZI DINI WAPEWA DAWA YA KUMALIZA MIGOGORO
Viongozi wa
dini wametakiwa kuwa
mstari wa mbele
kuwaelimisha Wananchi juu ya kulipa paumbele suala zima la mirathi jambo
ambalo litapunguza migogoro
katika Jamii.
Ushauri huo
umetolewa na wadau waliopata mafunzo juu ya utatuzi wa migogoro kwa njia ya
amani katika kongamano la jenga amani yetu lililoandaliwa na shirika la Seach
for Comman Ground lililofanyika Mgogoni Chake chake Pemba.
Wamesema
kuwa migogoro ya ardhi ndio tatizo kubwa ambalo linaonekana kuota mzizi katika familia nyingi hapa Visiwani.
Wameeleza
kuwa familia nyingi hazina tamaduni ya
kurithishana mali wanazoachiwa na wazazi wao pindi wanapofariki kitu ambacho ndicho
kinachochochea kuongezeka kwa migogoro
ya ardhi ndani ya Jamii.
‘’Kwa keli
tunatatizo tusifichane hatuna tabia ya
kurithishana, na hiyo inapelekea wengine
kukosa haki yao stahiki, hivyo nyinyi mashekha munadhima kubwa ya kutoa elimu juu ya hilo’’ walieleza wadau
wa amani.
Aidha wadau
hao wameliomba shirika la Seach for Comman Graund kuendelea kutoa elimu juu ya
utatuzi wa migogoro kwa njia ya mazungumzo jambo ambalo litaepusha uvunjifu wa Amani
Nchini.
Kongamano
hilo linalohusu umuhimu wa kutatua
migogoro kwanjia ya Amani liliwakutanisha
watu mbali mbali wakiwemo Masheha, Viongozi wa dini, Wanasiasa,
Wanahjarakati pamoja na wandishi wa habar.
Comments
Post a Comment