OFISI YA MUFTI YA NENA JUU YA WATU WENYE ULEMAVU.
Kauli hiyo
imetolewa na naibu katibu mufti ofisi ya Pemba Said Ahmad mara baada ya
kumtembelea mwalimu wa madrsatul juhudia Sada Khamis Hamad mwenye ulemavu wa
viungo mkazi wa Shumba vyamboni wilaya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Alisema
ziara hiyo ya kumtembelea mwalimu huyo imekuja kufuatia tarifa iliyotolewa na
vyombo vya habari ikiwemo mtandao wa Pemba Ya Leo Blog iliyonesha changamoto zinazo
mkabili mwalimu huyo ya ukosefu wa madrsa ya kufundishia wanafunzi wake.
‘’Kama ofisi
ya mufti tumeguswa na hilo na ndio mana tukaamua kuja kukuona na sisi tuweze
kukusikiliza kero zako ambazo zinakukabili katika madrasa yako’’ alisema sheikh
Said.
Alisema kwa
vile ofisi ya mufti ndio mlezi mkuu wa madrsa zote za quran watafanya jitihada
mbali mbali pamoja na kutafuta wahisani ili kuona amejengewa madrasa yake jampo
ambalo litatoa hamasa ya ufundishaji kwa mwalimu huyo.
Alisema jambo analolifanya mwalimu huyo wakike la kufundisha quran ni jambo la kuigwa na la kupigiwa mfano hivyo ni vyema jamii
kumuunga mkono kwa kumsaidia kwa misaada ya hali na mali ili aweze kuendeleza madrasa yake kwa maslahi ya makubwa ya watoto
na jamii kwa upana wake.
Akizungumza
mbele ya ugeni huo mwalimu huyo alisema kuwa changamoto kubwa inayomkabili
katika madrasa yake ni ukosefu wa sehemu salama ya kufundishia.
‘’Hapa
barazani ninaposomeshea panavuja mvua ikinyesha hatakama ni siku tatu wanafunzi
hulazimika kubaki nyumbani mpaka pale mvua itakapo pita’’ alieleza mwalimu.
Nao
wanafunzi wanasoma katika madrasa hiyo waliufurahia ugeni huo wakisema wamepata
matumaini kwamba utakua ni muarubaini wa
kupata ufumbuzi changa moto hiyo inayowakabili madrasani hapo.
Comments
Post a Comment