MTUHUMIWA AKATAA SHITAKA
NA FATMA HAMAD PEMBA.
Mahakama ya mkoa B iliopo Kusini Pemba imeghairisha kesi ya kuingilia kinyume na maumbile inayomkabili kijana Khamis Abdala Khamis marufu kirare mwenye umri wa [20] mkaazi wa Kangani wilaya ya Mkoani baada ya mtuhumiwa huyo kukataa kusomewa shitaka lake .
Kijana huyo wakati akiwa ametulia kizimbani na kusubiri asomewe shitaka lake aliambia mahakama hiyo kuwa hali yake sio mzuri anaomba kesi ighairishwe na ipangiwe siku nyengine.
‘’Mheshimiwa hakimu leo naumwa siwezi kukakaa hivyo naiomba mahakama yako ighairishe shauri hilo kwa leo’’ alieleza mtuhumiwa kirare.
Hakimu wa mahakama hiyo Muumin Ali Juma hakufurahishwa na kauli hiyo na kumueleza mtuhumiwa huyo kwamba hiyo ni haki yako na inahitajika upewe.
Lakini tu nikueleze leo shahidi ambae ni daktari amekuja wewe unasema unaumwa ila na siku akidharurika yeye tutamruhusu aende na safari zake utaendelea kukaa ndani atakapo rudi.
‘’ Usije ukasema mimi nitafuta kesi la hasha hilo sifanyi katu unajichelewesha mwenyeo utaendelea kukaa ndani’’ alieleza kwa msisitizo hakimu Mumin.
Na kesi hii itarudi tena mahakamani hapa siku ya tarehe 27/7/ 2022 kwa ajili ya kusikilizwa.
Mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo siku ya rehe 28/ 5/2022 ya smbili za usiku huko kangani Sokoni wilaya ya Mkoani bila ya halali na bila ya ridhaa ya walezi wake alimtorosha Mtoto wa miaka 10 kutoka sokoni alipokua amekaa na kumpeleka kwenye banda ambalo anaishi, na siku hiyo hiyo wakati wa 2; 7 usiku ulimuingilia kinyume na maumbile ambapo kufanya hivyo ni kosa kinyume na kifungu cha 115 cha sharia namba 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar.
Comments
Post a Comment