ALIEDAIWA KUWA NI BUBU SASA AANZA KUSEMA

 


NA FATMA HAMAD PEMBA.

Hatimae  Mahakama  ya  mkoa  B  Wete  yanza kusikiliza kesi ya ulawiti inayomkabili kijana  Nuhu Kombo Nuhu  miaka 19  mkaazi wa Kijichame wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba.

Mwendesha mashtaka wa Serikali Juma Mussa Omar amemuambia hakimu anaendesha  kesi hiyo kuwa shauri hilo lipo kwa ajili ya kusikilizwa na tulikua tunasubiri  cheti  kutoka kwa mtaalamu wa Afya kuthibitisha kwamba kijana huyo ni mgonjwa hawezi kuzunguza  ama ni kiziwi.

‘’Mheshimiwa hakimu tulitoa ombi  mahakama yako impeleke  hospitali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi  kama tayari basi tupo tayari kwa ajili ya kuskila’’ alisema DPP Juma.

Hakimu wa  Mahakama hiyo Abdulrahman  Ali  ameleza  kuwa  tayari tumesha pokea uthibitisho kutoka  Hospitali na majibu hayakuonesha  kwamba  mtuhumiwa  huyo  ana  ugonjwa wowote.

‘’Majibu yanaonesha kwamba si kibubu wala kiziwi anazungumza hivyo naighairisha hadi tarehe 25/7   na mashahidi waitwe tuanze kuwasikiliza’’  alieleza hakimu Abdulrahman.

Tukio hilo lilitokea tarehe 13/ 12/ 2021 majira ya sa moja asubuhi huko kijichame wilaya ya Micheweni mkoa wakaskazini  Kaskazini Pemba ambapo mtuhumiwa alimlawiti kijana mwenye ulemavu wa akili.

Ilidaiwa kuwa kufanya hyivyo ni kosa  kinyume na kifungu cha 116[1] cha sheria nambari 6/2018 sheria  ya Zanzibar.

 

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.