WAKULIMA WA KARAFUU MKOANI PEMBA WA NENA.
Wakulima wa
zao la karafuu wilaya ya Mkoani wameliomba
shirika la biashara la ZSTC kuweka mikakati madhubuti ili waweze kuwadhibiti wale wote wanao jishuhulisha na biashara ya ununuzi wa
karafuu mbichi.
Wamesema
uwepo wa watu wanao nunua karafuu mbichi za vikombe ni moja ya sababu kubwa inayochangia ongezeko la wizi wa zao
hilo.
Ushauri huo
wameutoa katika mkutano wa tathmini juu
ya zao la karafuu katika msimu wa mwaka
huu huko Zstc Mkoani wamesema asilimia kubwa ya wanaoiba karafuu wanaziuza kwa
wale wanao nunua karafu za vikombe, hivyo ni vyema watendaji wa Zstc kuwa
makini na watu hao ili kuepusha uharibifu, pamoja na wizi katika msimu wa mwaka huu.
‘’Mheshimiwa
mkuu wa mkoa kweli tunaumizwa tunaibiwa karafuu zetu na hawa wanunuzi wa karafuu
za vikombe ndio wanaosababisha tunaomba hilo mliangalie’’ walieleza wakulima.
Kwa upande
wake mkulima Zubeir Mohd Said amesema sababu inayowapelekea wakulima kuuza karafuu
mbichi ni ule ucheleweshwaji wa muda wa
kuanza kununua katika vituo vya Zstc.
Mapema mkuu
wa mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor
Masoud amewatoa hofu wakulima hao na kuwambia kua wataendelea kutoa adhabu
kali dhidi ya wale wote watakao
fanya vitendo vya uharibifu wa zao la karafuu
ambavyo vinapelekea uhujumu uchumi wa Nchi pamoja na wazalishaji.
Akitoa tathmini
ya utekelezaji wa zao la karafuu kwa mwaka 2021-2022 kaimu mkurugenzi mwendeshaji wa shirika
la Zstc Zanzibar
Ali Suleiman Mussa amesema jumla ya tani Elfu nane mia
tano na sita nukta
tatu Sifuri zilinunuliwa na
shirika hapa kisiwani Pemba katika msimu uliopita.
Comments
Post a Comment