JAMII YAHINIZWA KUITUNZA AMANI
NA FATMA
HAMAD PEMBA.
Wadau wa
ujenzi wa Amani
Kisiwani Pemba wametakiwa
kuendelea kuielimisha jamii juu
ya athari za migogororo
na weweze kujiepusha ndani
ya familia zao.
Wito huo
umetolewa na Afisa mdhamini ofisi ya rais tawala za mikoa na idara malum za
SMZ wakati akizungumza na wadau
waliopatiwa taluma ya ujenzi wa amani huko Green Folage Hotel iliyopo Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba.
Amesema
amani ndio msingi mkuu unaosababisha
maendeleo Nchini, hivyo ni
wakati kwa kila mtu kwa anafasi yake kuchukua hatua ya kuwaelimisha wenzake kuepuka kufanya mambo ambayo yanapelekea migongano na mifarakano isiyoyalima.
‘’Wadau wenzangu bado tunajukumu kubwa la kuisaidia jamii kuwafahamisha jinsi ya kutatuwa migogoro
kwa njia ya amani ili kuona wanaishi kwa kuvumiliana
na kusameheana bila ya kulipiziana
visasi ’’ alieleza Ofisa mdamini.
Aidha kwa
upande mwengine amewataka wananchi kutoa mashirikiano ya hali ya juu na kushiriki
kikamilifu zoeze la Sensa ambalo
linatarajiwa kufanyika mwezi wa nane
mwaka huu 2022.
Comments
Post a Comment