NUHU AENDELEA KULA BATA RUMANDE
Mahakama ya mkoa
B iliyopo Wete imeghairisha
shauri la Ulawiti
linalo mkabili kijana Nuhu Kombo
Nuhu mwenye umri
wa miaka 19 mkazi
wa Kijichame wilaya
ya Micheweni Mkoa
wa Kaskazini Pemba baada ya
mtuhumiwa kudai kuwa anaumwa na homa.
Mtuhumiwa
huyo ameiambia mahakama hiyo kuwa hajisikii vizuri
anaumwa hivyo anaiomba kughairisha
shauri hilo na apangiwe siku nyengine kwa ajili ya kusikilizwa.
Mwenedesha
mashtaka wa Serikali kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka DPP Juma Mussa Omar
amewambia mashahidi waliofika kwa ajili
ya kutoa ushahidi wao kwamba mtuhumiwa leyo kasema anaumwa
hivyo tukiendelea tutakua tunamnyima
haki yake .
‘’Kwa vile
mtuhumiwa kasema hayuko vizuri nawaomba murudi na musichoke muje tena siku
mutakayoitwa’’ alieleza DPP Juma.
Hakimu wa
mahakama hiyo amekubaliana na ombi hilo nan a kusema kuwa mtuhumiwa atarudi rumande hadi siku ya tarehe 3/ 8/
2022 kwa ajili ya kusikiliza mashahidi.
Tukio hilo
lilitokea tarehe 13/ 12/ 2021 majira ya sa moja asubuhi huko kijichame wilaya
ya Micheweni mkoa wakaskazini Kaskazini
Pemba ambapo mtuhumiwa alimlawiti kijana mwenye ulemavu wa akili.
Ilidaiwa
kuwa kufanya hyivyo ni kosa kinyume na
kifungu cha 116[1] cha sheria nambari 6/2018 sheria ya Zanzibar.
Comments
Post a Comment