WATU WENYE ULEMAVU WAIOMBA SERIKALI KUONDOSHA VIKWAZO KWENYE MIKOPO.
NA FATMA HAMAD,PEMBA
VIKUNDI vya Ushirika vya Watu wenye ulemavu Kisiwani Pemba vimeiomba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwaondeshea vikwazo kwenye suala la upatikanaji wa Mikopo inayotolewa kwa ajili ya kuwawezesha Wananchi kiuchumi ili kuona watu wenye ulemavu nawao wananufaika na fursa hiyo.
Hayo
yamesemwa na Omar Kombo Hamad kutoka kikundi cha Twamshukuru Allah kilichopo mbuzini na Fatma Salim Hamud wa kikundi cha Nia
njema kutoka Ole kianga cha watu wenye
ulemavu mara baada ya kumaliza mafunzo ya ya utengenezaji wa bidhaa mbali mbali
ikiwemo Mafuta ya mgando ya mwani, mafuta ya mkaratusi pamoja na Jiki huko Ole
mihogoni Chake chake Pemba.
Walisema ili kuona watu wenye ulemavu wananufaika
na fursa mbali mbali zilizomo kwenye Serikali, nivyema kupatiwa mkopo kwa mtu mmoja mmoja na isiwe lazima wawepo kwenye Vikundi vya
ushirika.
‘’Watu
wengine wenye ulemavu hawawezi kuingiza Pesa[akiba] mule kwenye hisa kwani
wengi hawana kazi ya kufanya mpaka tuwape sisi wazazi wao, hivyo tunaiomba
Serikali iangalie tena kwa jicho la pili kwani masharti ya mkopo wawe kwenye kikundi
ni shida kwa watu hawa,’’ walisema.
Walisema ni
vyema Serikali kuwapatia posho kila mwisho wa mwezi kama vile Pencheni ya Wazee
ili iweze kuwasaidia katika maisha yao .
Samba mba na
hilo wameiomba Serikali kuwapa kipaombele watu wenye ulemavu katika Sekta mbali
mbali ikiwemo ajira ili kuona nawao wanashika nyadhifa na kupata fursa zilizomo
kwenye Serikali yao.
Alisema watu
wenye ulemavu wamekuwa wakisahauliwa katika fursa mbali mbali za kimaendeleo,
hivyo wameamua kuleta mradi huu ili kuona nwao wanashiriki katika nyanja mbali
mbali mbali jambo ambalo litawafanya nawao waisha katika maisha mazuri kama
watu wengine wasio na ulemavu.
‘’Tuliona
miradi mingi inayoletwa na Serikali pamoja na mashirika binafsi imekuwa
ikiwacha nyuma watu wenye ulemavu, hivyo tumeleta mradi huu wa kijaluba na
kuwapatia mafunzo ya utengenezaji wa vitu mbali li ili kuwapunguzia hali ngumu za kimaisha,’’
alieleza.
Comments
Post a Comment