NA
FATMA HAMAD,PEMBA
Wakulima wa mwani wametakiwa kulima kilimo cha kisasa ili waweze
kuzalisha zao hilo kwa wingi.
Ushauri huo umetolewa na Afisa Mazimgira kutoka idara ya
mazimgira na Ofisi ya makamo wa kwanza wa Rais Hassan Hamad Hassan wakati
akizunumza na wanavikundi vya ulimaji wa mwani huko kilindi Chake chake
Pemba.
Amesema Sera ya Serikali ya Uchumi wa buluu ni kuhakikisha
inawainua wakulima wa mazao ya baharini ili waondokane na umaskini.
Hivyo alisema ni wakati kwa Wakulima wa Mwani kuondokana na
kilimo cha zamani, na badala yake walime kilimo cha kisasa (walime kwa ajili ya
biashara) jambo ambalo litawawezesha kuvuna zao hilo kwa wingi na
kujipatia kipato.
"Niwaombe Wakulima mbadilike msilime kimazoe, mlime kilimo
cha kisasa na mlime Mwani kwa ajili ya biashara, msilime
panatosha,"alisema.
Sheha wa Shehiya ya kilindi Nassor Muhammed Khamis aliwataka wakulima hao
waliopatiwa mafunzo kuyatumia mafunzo hayo ili waweze kulima kilimo chenye
ubora ambacho kinaendana na Soko la Dunia.
Nao badhi ya washiriki hao wameishukuru Serikali kwa kuwapitia
Elimu juu ya ulimaji wa mwani wa kisasa pamoja na vitendea kazi, huku wakiahidi
kuongeza jitihada ya kuzalisha na kuboresha kilimo Chao.
Mafunzo hayo waliopatiwa wakulima wa mwani wa kikundi cha Nyumba nyeupe na Dongoni
Coperative ni utekelezaji wa mradi wa SAPPHIRE wenye Lengo la kusimamia
mazingira ya pwani katika maeneo ya PECCA ambao unaendeshwa na Ofisi ya Makamo
wa kwanza wa Rais pamoja na Idara ya Mazingira.
Comments
Post a Comment